Breaking News

Zoezi la ugawaji wa Miguu bandia limeendelea


Zoezi la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza leo ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.

Katika awamu ya pili iliyoanza leo zaidi ya Walemavu 108wamepatiwa Miguu ya kisasa ya Bandia ambayo inakadiriwa Mguu mmoja unagharimu kiasi cha shilling million 2 hadi 3 ambapo yote kwa pamoja ni Shilling Million 324,000,000 lakini kwa jitiada za RC Makonda wamepatiwa Miguu hiyo Bure.

Katika awamu ya Kwanza jumla ya Wagonjwa 35 wa kisukari walipatiwa miguu ya kisasa ya bandia yenye thamani ya Shilling million 157 kutoka CCBRT na kufanya jumla ya walemavu waliopatiwa miguu hiyo kufikia 143 yenye thamani ya Million 481 Bure.

Baadhi ya Walemavu waliopatiwa Miguu hiyo wamemshukuru RC Makonda kwa moyo wa pekee wa kuwajali wananchi wake kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii ambapo wamesema kwa sasa wataenda kufanya kazi na kuachana na utegemezi.

Aidha wameishukuru kampuni ya Kamal Group kwa kumuunga mkono RC Makonda kutimiza maono yake ya kuwawezesha walemavu kupata miguu ya kisasainayowawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

No comments