POLISI DAR YAKANUSHA HABARI YA KUKAMATA WAVAA VIMINI, MILEGEZO NA WANYOA VIDUKU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekunusha taarifa ya kukamata watu wanaovaa vimini na kunyoa mtindo wa kiduku.
Hatua hiyo inakuja baada ya gazeti la kila siku la Nipashe January 17
(jana) kutoka na kichwa cha habari; Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa
viduku.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa
alisema taarifa hiyo haina ukweli wowote kwani mwandishi ameandika kitu
ambacho hakukisema.
“Nilitaka nitoe ufafanuzi nikikanusha haya ambayo yameandikwa
hayakusemwa na Jeshi la Polisi, ameyasema mwenyewe mwandishi kwa
interest yake na sana alichokuwa anatafuta ni umaarufu wa stori.
Mambosasa alisema hakuna sheria yoyote inayowazuia watu kuvaa nguo fupi
na kwamba alichokisema Rais Magufuli ni kwamba anachukizwa na wasanii
wanaovaa nusu uchi na kuoneshwa katika vituo vya Runinga,kitu ambacho ni
kinyume na maadili yetu.
"Kwa kuwa jambo hilo ni machukizo na halivunji sheria za nchi ni vigumu
kwa Polisi kuanzisha msako, labda watu hao tuwakute wakifanya biashara
ya ukahaba." Alisema Mambosasa na kuongeza;
“Ninamtaka sasa mwandishi arudi kwa watanzania aombe radhi ili kuondosha
usumbufu uliojitokeza, nimepigiwa simu kuanzia jana(juzi) toka maeneo
mbali mbali kwa jambo ambalo kimsingi halijafanywa na Jeshi la Polisi.”
No comments