CHADEMA YAANZA MWAKA NA NGUVU YA AJABU
Katibu wa Jimbo la
Ukonga Daniel Ruhuro (kushoto) akimkabidhi Katibu wa Kamati tendaji Kata ya
Chanika, Charles Sangiwa jijini Dar es Salaam leo barua yenye maelekezo ya uenezi
wa Chama (Chadema ni msingi) ambayo ina ajenda ya kueneza sera za Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutafuta wanachama wapya jimboni.Makabidhiano
hayo yamefanyika katika Ofisi ya Chama Gongo la Mboto.
Mwenyekiti wa Kamati
tendaji wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Pugu,Maira Otieno(kulia)
akipokea barua yenye maelekezo ya uenezi wa Chama (Chadema ni msingi) kutoka kwa Katibu wa Jimbo la Ukonga Daniel
Ruhuro jijini Dar es Salaam leo.Barua hiyo inaajenda ya kueneza sera za Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutafuta wanachama wapya jimboni.Makabidhiano
hayo yamefanyika katika Ofisi ya Chama Gongo la Mboto.
Mwenyekiti wa Kamati
tendaji Kata ya Mzinga Chacha Momba (kushoto) akipokea barua yenye maelekezo ya
uenezi wa Chama (Chadema ni msingi) kutoka
kwa Katibu wa Jimbo la Ukonga Daniel Ruhuro jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati
tendaji Kata ya Ukonga Deo Malongo (Kushoto) akipokea barua yenye maelekezo ya uenezi wa Chama
(Chadema ni msingi) kutoka kwa Katibu wa
Jimbo la Ukonga Daniel Ruhuro jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa Tawi la
Kitunda Kati Kamanda Moses Kidew (kulia) akipokea barua yenye maelekezo ya uenezi
wa Chama (Chadema ni msingi) kutoka kwa Katibu
wa Jimbo la Ukonga Daniel Ruhuro jijini Dar es Salaam leo kwa niaba ya Mwenyekiti
wa Kamati tendaji Kata ya Kitunda Kamanda Nelson Barongo.
Katibu wa Kamati ya
utendaji Kata ya Gongo la Mboto Kamanda Amon Matiko (kulia) akipokea barua yenye
maelekezo ya uenezi wa Chama (Chadema ni msingi) kutoka kwa Katibu wa Jimbo la Ukonga Daniel
Ruhuro jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa Kamati ya
utendaji Kata ya Zingiziwa Salma S. Kondo (kulia) akipokea barua ya maelekezo ya zoezi
la Chadema ni Msingi kutoka kwa Katibu
wa Kamati ya Utendaji Jimbo la Ukonga Kamanda Daniel Ruhuro jijini Dar es
Salaam leo.
Mwakilishi wa Kamati
tendaji Kata ya Majohe Kamanda Sebastian Bendera (kulia) akipokea barua
ya maelekezo
Mwakilishi wa Kata ya
Kivule Kamanda Chacha Marwa (kulia) akipokea barua
Katibu wa Kamati ya
utendaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Jimbo la Ukonga Kamanda Daniel
Ruhuro (kushoto) akisema jambo baada ya kukabidhi barua za maelekezo ya zoezi
la Chadema ni Msingi kwa Viongozi wa Kata mbalimbali ndani ya Jimbo la Ukonga
jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa Kata
mbalimbali Jimbo la Ukonga wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa Jimbo la
Ukonga Kamanda Daniel Ruhuro baada ya kupokea barua zenye maelekezo ya zoezi la
Chadema ni Msingi kama ilivyoelekezwa na uongozi wa Chama ngazi ya Juu.
Na mwandishi wetu
Leo Viongozi wa Kamati
tendaji za Kata ndani ya Jimbo la Ukonga wamefika Ofisi ya Jimbo Gongo la mboto kuchukua barua za maelekezo ya
zoezi la Chadema ni Msingi kama lilivyoelekezwa na Chama kutoka uongozi wa juu
kupitia kwa Makatibu wa Jimbo
Mnamo saa 4:30 Katibu
wa Jimbo la Ukonga Kamanda Daniel Ruhuro Manumbu alikuwa tayari amekwisha
wasili ofisi ya Chama cah Demaokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ukonga
kwa ajili ya kuwapatia viongozi hao wa Kata mbalimbali barua hizo zenye
maelekezo kama ilivyoelekezwa na uongozi wa juu wa Chama hicho
Viongozi wa Kata
waliofika kwa wakati kama walivyojulishwa jana na Katibu Ruhuro ni:-
(1). Lucas Maira
Mw/kiti Kamati tendaji Kata ya Pugu
(2). Deo Malongo
Mw/kiti Kamati tendaji Kata ya Ukonga na Samson Kilemwa Katibu wa Kamati
tendaji Kata ya Ukonga
(3). Nyakisagane
Mw/kiti, Samwel Simeu Katibu Mwenezi, Amon Matiko Katibu Kamati tendaji Kata ya
G'mboto
(4). Salma S. Kondo
Katibu Kamati tendaji Kata ya Zingiziwa
(5). Sebastian Bendera
Mjumbe mwakilishi Kata ya Majohe
(6). Charles Sangiwa
Katibu Kamati tendaji Kata ya Chanika
(7). Chacha Momba
Mw/kiti Kamati tendaji Kata ya Mzinga
(8). Nelson Muro/Diblo
Katibu Mwenezi Kata ya Kitunda akiwa ameongozana na Kamanda Moses Kidew Katibu
wa Kamati tendaji Tawi la Kitunda Kati
(9). Chacha Marwa
mjumbe mwakilishi Kata ya Kivule alietumwa na Mw/kiti wa Kata Kamanda
Gisiri
(10). Adolf Balebi
Mw/kiti kamati tendaji Kata ya Kipunguni
Kwa barua hizo katibu
amesisitiza zoezi la Chadema ni Msingi litekelezwe kwa wakati na kwa ufanisi
mkubwa kwani vifaa vya uenezi tayari vipo na watakabidhiwa maeneo wakati kazi
hiyo na kutafuta wanachama wapaya ikiendelea kwenye Kata, Matawi na kwenye
Misingi yote ndani ya Jimbo la Ukonga
No comments