RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MPIGAPICHA ATHUMAN HAMIS
Rais Mstaafu ya Awamu ya Nne Dr.
Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mpiga picha Mkuu
wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi katika maziko yaliyofanyika Makaburi ya
Kisutu jijini Dar es Salaam.
RAIS Mstaafu
wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya wananchi wa Dar es
Salaam katika mazishi ya aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa magazeti ya Serikali ya
Habari Leo na Daily News Athuman Hamis yaliyofanyika katika
Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu
Dk. Jakaya Kikwete katika mazishi hayo alikuwa ameongozana na
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harson Mwakyembe, Viongozi wa
Serikali, Wahariri, wanaandishi wa habari pamoja na wapiga picha za
habari katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Mauti ya mpigapicha
huyo yalimkuta jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
Kabla ya
mazishi hayo, nyumbani kwa marehemu Athumani Hamis Sinza Madukani ,
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya TSN, Dk.Jim Yonas amesema, Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda mbali ya kuguswa na kifo cha Athuman Hamis pia ameahidi
kuijengea nyumba familia ya marehemu itakayokuwa na vyumba vinne.
“Nilikuwa nazungumza
na Mkuu wa Mkoa wetu wa Dar es Salaam na ameniambia kuwa ofisi yake itajenga
nyumba ya vyumba vine kwa ajili ya familia ya marehemu Athuman Hamis,”amesema
Dk Yonas.
Pia amemueleza
marehemu Hamis kuwa enzi za uhai wake alikuwa mchapakazi hodari na licha ya
kuwa na matatizo ya kiafya bado aliipenda kazi yake.
Amesema Athuman
Hamis ameacha pengo kubwa katika tasnia ya habari na kuna mengi ya kujifunza
kutoka kwake hasa kwa wapiga picha wa vyombo vya habari nchini.Akizungumza
baada ya kumzika marehemu Hamis , Imamu wa Msikiti wa Sinza Maijiku Sheikh
Mohamed Suileman amesema enzi za uhai wake Hamis alikuwa ni mcha Mungu na
alipenda kufanya ibada.
Sheikh wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema Athuman Hamis wakati wa uhai wake
kabla ya kupata kupata matatizo ya ajali alikuwa ni mtu mwenye kupenda
kufanya ibada.
No comments