Makamu wa Rais Akagua Maendeleo ya Ujenzi wa Miradi ya Ukuta wa Bahari Katika Eneo la Kigamboni na Ocean Road
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Mradi na Miundo Mbinu wa UNOPS Bw. Bernard Odhuno wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameketi kwenye moja ya sehemu za kupumzikia pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba(kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500.
Waziri nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Ocean Road.
Ujenzi wa Ukuta wa bahari katika eneo la umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema mazingira yanatuadhibu kutokana na uharibifu unaofanywa na mwanadamu.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa ukuta wa bahari katika eneo la Kigamboni na Ocean Road jijini Dar es Salaam.
Akihutubia wananchi waliojitokeza katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho ukuta wenye urefu wa mita 500 unajengwa sambamba na sehemu za kupumzikia, Makamu wa Rais alisema “ tumeharibu mazingira na mazingira yanatupa adhabu lazima sasa turudi wote tuwe rafiki wa mazingira, turekebishe pale tulipoharibu, turekebishe pale tulipokosea ili mazingira yarudi tena yawe rafiki yetu”
Makamu wa Rais alisema kuwa uamuzi wa kufanya miradi ya kujenga ukuta wa bahari ni kuzuia bahari isiendelee kula ardhi.
Makamu wa Rais alisema pamoja na kujenga Ukuta huo unategemewa kudumu kwa miaka zaidi ya 70 , pia wamejenga mitaro kwa ajili ya kuzuia maji ya mvua yasilete madhara katika maeneo ya Ilala na Temeke.
Wakati huo huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema uharibifu wa mazingira ni janga la kitaifa hivyo alimpongeza Makamu wa Rais kwa kupaza sauti katika suala zima la utunzaji wa mazingira.
Vilevile Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amesema mkoa wa Dar es salaam utaendelea na kampeni ya kupanda miti inayojulikana kama Mti Wangu kwani kampeni hiyo ilikuwa moja ya maelekezo ya Makamu wa Rais.
No comments