Breaking News

Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu Azindua Mpango Mkakati wa Miaka 3 wa Taasisi ya Taaluma ya Afya ya Jamii Afrika.

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika leo jijini Dar es salaam.
 Mwasisi wa Taasisi  ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika  Dkt. Mary Sando leo akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.
Picha na Wizara ya Afya.

Dhima ya Taasisi  ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika (AAPH) ni kushirikiana na Seikali  na wadau wengine wa afya kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu afya ya mama na mtoto,masuala ya afya na lishe,magonjwa yasioambukizwa na yale yanayoambukiza.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa tatu kushoto akionesha kitabu cha mpango mkakati wa miaka 3 wa Taasisi ya Taaluma ya afya ya jamii Afrika pamoja na Mwasisi wa Taasisi hiyo Dkt. Mary Sando wa kwanza kushoto wakati wa uzinduzi wa mpango huo leo jijini Dar es salaam.

No comments