Breaking News

WAITARA ATIMIZA AHADI YAKE KWA KANISA KATHOLIKI LA MJI MPYA MAJOHE RELINI

Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Parokia ya Mji Mpya Majohe Relini  ya Kanisa Katholiki,Alfred Owino Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo. Huu ni mwendelezo wa Mbunge kutekeleza yali aliowaahidi wananchi wake ndani ya Jimbo.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara akizungumza jambo na waumini wa Parokia ya Mji Mpya Majohe Relini  ya Kanisa Katholiki (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam jana baada ya kukabidhi Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Parokia ya Mji Mpya ya Kanisa Katholiki,Alfred Owino akitoa shukrani zake za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara baada ya kukabidhiwa Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo lililopo Mji Mpya Majohe Relini  jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule,Innocent Kashumba (kushoto) akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara(katikati) madarasa ya Shule ya Msingi ya Kanisa Katholiki ambayo yamekamilika na yasiyokamili baada ya kukabidhiwa Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) na Mbunge huyo kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo lililopo Mji Mpya  Majohe Relini jijini Dar es Salaam leo.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara (katikati) akiteta jambo na Kamati ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa Katholiki lililopo Mji mpya Majohe Relini  katika hafla ya kukabidhi Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Kwaya ya Kanisa Katholiki (RC) Mji Mpya Majohe  Relini wakiimba wimbo baada ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara kukabidhi Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Madarasa ya shule hiyo mpya yanayoendelea kujengwa.

Baadhi ya Waumini wa wa Parokia ya Mji Mpya  ya Kanisa Katholiki wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara (hayupo pichani) katika hafla ya kukabidhi Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo.

Katibu wa Parokia ya Mji Mpya Majohe Relini  ya Kanisa Katholiki Benedict Kelela nae akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara (hayupo pichani) baada ya kukabidhi Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa Katholiki lililopo Mji mpya Majohe Relini  katika hafla ya kukabidhi Hundi yenye thamani ya Shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.


No comments