Breaking News

Brigitte awakumbuka walemavu wa ngozi


Na Mwandishi wetu
Kwa mara ya kwanza katika historia ya maonyesho ya mitindo ya mavazi nchini, watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)  juzi ijumaa walipanda jukwaani kufanya maonyesho hayo chini ya uratibu wa  Taasisi ya Miss Tanzania 2012 , Brigitte Alfred Foundation (BAF) kwa kushirikiana na ofisi ya Ubalozi wa Uturuji nchini.

Maonyesho  hayo yalihudhuriwa na warembo na watu maarufu mbalimbali yalijulikana kwa jina la “My Skin My Pride” yalifana sana huku wabunifu nao wakionyesha ufundi mkubwa katika staili mbalimbali za mavazi. Wabunifu hao ni Annisa, Enjipai, Lavo Delama, Jacques Collection na   Mac Couture. 

Mke wa Balozi wa Uturuki nchini, Yesim Ali  alisema kuwa wameamua kufanya maonyesho hayo kufuatia kuguswa na watu wenye albino ambao wanauwa kutokana na imani potofu.

Yesim alisema kuwa alitembelea shule ya Buhangija, Shinaya na kuona juhudi za mrembo Brigitte aliyefanikisha kujenga mabweni ili kuwalinda na kuendelea kupata elimu bila ya kuwa na wasiwasi.

Alisema kuwa wameungana na Brigitte katika vita hiyo na kuomba wanao jihusishwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa upande wake, Brigitte alisema kuwa ataendelea na kampeni yake hiyo ili kuhakikisha kuwa jamii inaungana na kutokomeza mauaji hayo.

“Nilianzisha kampeni hii nikiwa miss Tanzania na nashukuru kuwa jamii imeniunga mkono japo kuna watu wachache wanaendelea na mila potofu,” alisema Brigitte.

Miss Tanzania 2000, Jucqueline Mengi alipongeza juhudi za Brigitte na kuunga mkono kampeni hiyo.
Pia Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari  na Miss Tanzania 2008, Nasreen Karim wameunga mkono hatua hiyo ya Brigitte na kuomba jamii kuungana naye ili kukomesha mauji ya albino.

Mwisho…

No comments