Breaking News

WAITARA ASHIRIKI KATIKA KIKAO CHA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KATI YA SHULE YA SEKONDARI PUGU NA WANANCHI WALIOKUWA JIRANI

Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (watatu kulia) akiangalia mchoro wa mipango miji  ya Shule ya Sekondari Pugu  pamoja na wataalam wa idara ya ardhi Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo katika kikao cha kujadili malalamiko yaliyopelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na uongozi wa Shule ya Sekondari Pugu baada ya wananchi waliojirani na Shule hiyo kuvamia eneo la Shule na kujenga nyumba . Pia kikao hicho ni agizo lililotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu alipotembelea shuleni hapo tarehe 9 novemba 2017.




Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (kulia) akiwa pamoja na wataalam wa idara ya ardhi Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo katika kikao cha kujadili malalamiko yaliyopelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na uongozi wa Shule ya Sekondari Pugu baada ya wananchi waliojirani na Shule hiyo kuvamia eneo la Shule na kujenga nyumba . Pia kikao hicho ni agizo lililotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu alipotembelea shuleni hapo tarehe 9 novemba 2017.

Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (kulia) akizungumza jambo  na wataalam wa idara ya ardhi Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo katika kikao cha kujadili malalamiko yaliyopelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na uongozi wa Shule ya Sekondari Pugu baada ya wananchi waliojirani na Shule hiyo kuvamia eneo la Shule na kujenga nyumba.

Wataalam idara ya ardhi Manispaa ya ilala wakiwa katika kikao cha kujadili malalamiko yaliyopelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na uongozi wa Shule ya Sekondari Pugu baada ya wananchi waliojirani na Shule hiyo kuvamia eneo la Shule na kujenga nyumba.

Na mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo Ukonga Mhe Mwita Waitara ahudhuria kwenye kikao cha wataalam wa idara ya ardhi Manispaa ya Ilala kilichofanyikia Shule ya Sekondari Pugu kutokana na malalamiko yaliyopelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na uongozi wa shule hiyo baada ya wananchi waliojirani kuvamia eneo la Shule na kujenga nyumba 

Pia kikao hicho ni agizo lililotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu alipotembelea shuleni hapo 09 Novemba 2017. 

Mbunge alishauri mawasiliano kati ya Manispaa, Shule na wananchi waliojirani na Shule yafuate taratibu za kisheria ili mahusiano mazuri yaendelee kuwepo kati ya wananchi na taasisi za Umma mfano; Shule, Hospitali n.k

Walioshiriki kikao hicho ni Watu wa idara ya ardhi Manispaa ya Ilala,Diwani Kata ya Pugu Mhe.Mphuru, Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Mtendaji Kata ya Pugu, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bombani pamoja na Mratibu wa Elimu Kata ya Pugu.

No comments