Kamati ya Bunge Yaipongeza DAWASA/DAWASCO Kwa kazi Nzuri ya Kusimamia Miradi ya Maji
KAMATI ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, imeipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASCO), kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na DAWASA na DAWASCO Dar es Salaami na mkoa wa Pwani leo Januari 20, 2018, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, alisema. Kazi iliyofanyika ni kubwa na Kamati imeona jinsi gani fedha za serikali zimetumika.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema, miradi mingi inatekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka India, lakini Kamati imebaini kuwa kila kitu kinafanywa na makampuni ya kutoka India, jambo ambalo sio sahihi sana.
“Inawezekana kuna mahali ambapo tumezidiwa, au kujichanganya, na kama ni kwenye component ya huo mkopo iliandikwa, kuna jambo la kuangalia na kujadili.” Alisema Mhe. Papian.
Aidha Mhe. Papian alisema Kamati inashauri kuwa watendaji wa ndani (Wakandarasi) wanapomaliza hii miradi basi vijana wa Kitanzania lazima wawe wameshajua na kufundishwa na wajifunze kila kitu ili waweze kuendesha miradi hii kikamilifu.
Ziara ya Kamati hiyo ilianzia makao makuu ya DAWASA, ambapo Kamati ilipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA na DAWASCO, na kasha walipata fursa ya kutembeela baadhi ya miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji ya Changanyikeni, Salasala, vituo vya kusukuma maji vya Makongo na Salasala.
Kamati pia ilitembelea eneo la utandazaji mabomba ya kusambaza maji huko Mpiji Machimbo na kumalizia ziara yao kwa kutembelea mitambo ya maji ya Ruvu chini na Ruvu Juu.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo alisema, Mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na katika Miji ya Bagamoyo na Kibaha na tayari umefikia asilimia 72.2 kukamilika.
“Mradi huu unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), ulianza rasmi Machi mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2018.” Alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu kazi zinazofanyika kwa sasa, Mhandisi Mwang’ingo alitaja kuwa ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi kati ya lita za ujazo milioni 3.0 hadi milioni 6.0 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vine vya kusukuma maji na ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa za kusukuma maji 16.
Kazi nyingine ni pamoja na ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji mabomba yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilomita zipatazo 477.
“Maeneo yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu.” Alifafanua.
Aidha maeneo mengine yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba Mawili na Msigani na maeneo hayo yote yanapata huduma ya maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu uliozindulkiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Juni 21, 2017.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Bw.;aston T. Msongole, alisema ni nia ya DAWASA kuhakikisha maeneo yote ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji hususan baadhi ya maeneo ya wilaya mpya ya Kigamboni, ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikia.
“Tayari tumechimba visima virefu vyenye uwezo wa kutoa maji mengi ya kumaliza tatizo la ukosefu wa maji kwenye maeneo hayo lakini tatizo ni uhaba wa fedha za kutengeneza mfumo wa kuyasambaza maji hayo kwa walaji” Alisema Bw.Msongole.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Daniel; Nsanzugwanko, (katikati) akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo, (kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, walipotembelea mtambo wa maji wa Ruvu Juu, Mlandizi mkoani Pwani.
Kaimu Mwewnyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kushoto) na mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Nsanzugwanko, (katikati), wakimsikilzia Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye eneo la ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji wa Salasala.
Taswira ya maendeleo ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi na kusambaza maji la Salasala ukiwa umefikia hatua ya ufunikaji kabla ya kumwaga zege.
Mafundi wakisuka non do tayari kwa kumwaga zege kwenye tenki la Salasala.
Modester Mushi (kushoto), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA akiwa na Afisa Habari na UHusiano wa Jamii Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bi.Mecky Mdaku wakati wa ziara hiyo ya Kamati ya Bunge huko Salasala.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, (kushoto), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya. |
Kamati ikipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA/DAWASCO mwanzoni mwa ziara hiyo.
Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya, akigawa taarifa ya DAWASA kwa wajumbe wa Kamati. |
Baadhi ya wajumbe wa Kamati, wakisikiliza taarifa hiyo.
Mjumbe wa Kamati, Mhe,Kuntyi Yusuph Majala, akizunhgumza wakati wa Kamati ikipkea taarifa.
Mhandisi Mwangi’ngo, akitoa taarifa ya utendaji ya DAWASA.
Picha ya pamoja ya Kamati na watendaji wa DAWASA/DAWASCO na wajenzi.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
No comments