DK. MNDOLWA AKABIDHIWA RASMI OFISI JANA, AAHIDI KUUNDA KAMATI KUTAFUTA UFUMBUZI DHIDI YA KUMOMONYOKA KWA MAADILI KATIKA JAMII YA KITANZANIA
Mwenyekiti
Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi
nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya
hiyo, Dk. Edmund Mndolwa,jana, Makao Makuu ya Jumuiya jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar
Abdallah Haj Haidar.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa
Jumuia hiyo Seif Shabani Mohamed alipowasili Makamo Makuu ya Jumuiya hiyo kwa
ajili ya makabidhiano hayo.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa akisalimiana na Naibu Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Najma Giga wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Mndolwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuia
hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Makamu Menyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Abdallah Haj Haidar.
Mwenyekiti
mstaafu wa Jumuiya ya Wqzazi Tanzania Abdallah Bulembo akionyesha Katiba ya
Jumuiya hiyo kabla ya Kumkabidhi Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania
Dk Edmund Mndolwa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hizo Zanzibar Abdallah
Haj Haidar.
Mwenyekiti
Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi
nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo, kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya
hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, jana, Makao Makuu ya Jumuiya jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani
Mohammed na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar Abdallah Haj
Haidar.
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti mpya wa
Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuunda Kamati ya
kutathmini namna Jumuiya hiyo inakavyolishughulia kwa ufanisi tatizo la
kuporomoka kwa maadili katika jamii hapa nchini.
Dk. Mndolwa ametoa
ahadi hiyo leo, hayo wakati akikabidhiwa rasmi Ofisi na Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo, hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya
Wazazi Tanzania jijini Dar es Salaam.
"Katika hotuba
ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli alitutaka sisi viongozi wa Jumuiya
hii tusikae kimya wakati vitendo vya kuporomoka kwa maadili katika jamii
ikiwemo wasanii wa kike kuonyesha sehemu za miili yao zinazotakiwa kusitiriwa.
Sasa hili ni agizo lazima mimi na viongozi wenzangu tulipe kipaumbele katika
kulifanyika kazi.
Kwa hiyo baada ya
kukabidhiwa rasmi ofisi leo hii, miongoni mwa mipango yangu Kama Mwenyekiti ni
Kuunda Kamati itakayojikita kwa undani kuhakikisha tunapata njia bora za
kudhibiti kuporomoka kwa maadili katika jamii ya Watanzania", alisema Dk
Mndoldwa. Alisema, pia atahakikisha katika zama za uongozi wake, Jumuiya
ya Wazazi inainuka na kujitegemea vya kutosha kiuchumi ili iondokane na adha ya
kuwa ombaomba.
"Jumuiya hii
ianazo mali nyingi, kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha fedha zinazotokana na
mali au miradi hii zinaingia kwenye hazina ya Jumuia badala ya kupotelea
mifukoni mwa wajanja wachache, tukifanikiwa kuthibiti bila shaka tutakuwa na
fedha za kutosha", alisema Dk. Mndolwa.
Akimzungumzia
Bulembo, Dk Mndolwa amesema, alikuwa kiongozi bora ambaye ameisaidia kwa kiasi
kikubwa Jumuiya ya Wazazi, na kwamba katika jitihada zake ameiboresha Jumuia
hiyo kwa karibu asilimia tisini.
"Nimejifunza
mambo mengi kwa Bulembo, mojawapo ni uvumilivu, huyu ni mvumilivu kiasi kwamba
itanibidi kuiga uvumilivu wake ili na mimi nistaafu kwenye Jumuiya hii nikiwa
safi kama yeye," Alisema Dk. Mndolwa.
Kwa Upande wake
Bulembo aliwataka viongozi wapya wa Jumuiya hiyo kuthamini sana Waaandishi wa
habari kwa kuwapa ushirikiano kila unapohitajika na kwamba yupo tayari kutoa
ushauri pale utakapohitaji.
Aliwaasa viongozi
wapya kuendeleza mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita huku wakiachana na
mabaya yaliyofanyika wakati huo.
"Namna nzuri ya
kuongoza ni kuwa karibu na unaowaongoza, msikae nao mbali mnaowaongoza na ikiwa
kutakuwa na jambo miongozi mwenu viongozi ambalo haliendendi vizuri utatuzi
wake uwe kwenye vikao si kwingineko", Alisema Bulembo.
No comments