WATEJA WA AIRTEL WAZIDI KUJIVUNIA ZAWADI KEMKEM.
Kampuni ya simu za mkokoni Airtel Tanzania leo imewazadia washindi 2,000 wa droo ya Pili wa promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti kwenye droo iliyochezeshwa leo katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa droo hiyo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “wateja wa Airtel 2000 wameweza kujishindia bando ya 1GB kila mmoja, lakini siku ya Jumatatu washindi wengine 2,000 pamoja na washindi 10 watajishindia Smartphone za BURE”
Droo ya hiyo ya SHINDA NA SMATIKA imechezeshwa chini ya usimamizi wa afisa kutoka boda ya michezo ya kubahatisha Bw, Humud Semvua
Baada ya promosheni hiyo washindi wote 2,000 wametumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kufahamishwa kuhusu ushindi wao pamoja na kuwekewa kila mmoja GB1 ya intaneti bure hapohapo.
Mmbando alifafanua kuwa hii ni droo ya pili ambapo bado droo zitaendelea kuchezwa kila Jumatatu, Jumatano, na Ijumaa kwa muda wote wa mwezi wa pili.
“cha muhimu kwa mteja ni kuendelea kununua na kutumia Yatosha intaneti haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti piga tu *149*99# halafu changua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo atanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu.”
ukiwa mtumiaji mzuri droo kubwa ya jumatatu kutakuwa na washindi 10 huku watano wakishinda simu za smatiphone na 5 wakijishindia moden.” alisema Mmbando
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na wa habari wakati Airtel Ilipochezesha droo ya pili ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ambapo washindi 2000 tena kila mmoja alijishindia 1GB. (Kushoto) ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Humud Semvua na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na mmoja kati ya washidi wakati Airtel Ilipochezesha droo ya pili ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ambapo washindi 2000 tena kila mmoja alijishindia 1GB. (Kushoto) ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Humud Semvua na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar
No comments