Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Rc Makonda azisimamisha shughuli zote za mabaraza ya kata
Shughuli zote za Mabaraza ya ardhi ya kata katika Mkoa wa Dar es Salaam zimesimamishwa Kwazia leo February 10,2018 kufuatia kuonekana kuwa hazina uwezo wa kusikiliza kesi za ardhi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa huo Mhe. Paul Makonda katika mkutano wa mrejesho wa malalamiko ya wananchi waliofika katika ofisi ya Mkuu huyo kupatiwa msaada wa kisheria zoezi lililodumu takribani siku tano.
Amesema mabaraza mengi ya Kata yamekuwa yakilalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi na kutenda haki kwa walengwa waliowasilisha mashauri yao katika ofisi hizo.
"Mabaraza yote ya ardhi ya Kata katika Mkoa wangu kwanzia leo Ferbuari 10, nasimamisha shughuli zote,na kesi zote zilizopo katika mabaraza hayo ziwasilishwe kwa makatibu Tarafa "Amesema Rc Makonda.
Aidha Rc Makonda amewavua madaraka wakuu wa Idara ya ardhi katika manispaa za Ubungo na Ilala kutokana na kushindwa kutoa takwimu sahihi za mashauri ya ardhi yaliyopo katika wilaya zao.
Amewaagiza wakurugenzi kuwapangia kazi nyingine wakuu wa idara hao kutoka katika manispaa hizo kwani wameonekana kuwa wazembe na kutowajibika ipasavyo katika nafasi zao na kuharibu sifa ya Serikali.
"Wakurugenzi naomba Kwanzia leo muwapangie kazi nyingine hawa kwani hawana sifa za kuwa katika nafasi hizo, Hawana takwimu sahihi za mashauri waliosikiliza katika halimashauri zao hatuwezi kuendelea kuwa na watu wazembe,wasiowajibika wanaaribu sifa ya Serikali ya Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli "Amesema Makonda.
Wakuu wa idara ya ardhi waliovuliwa nyazifa hizo ni Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Ubungo Khamisi Songwe ambaye alishindwa kutoa takwimu ya kesi zilizopo katika halmashauri hiyo na kusema hakuna kesi yoyote ya ardhi pamoja na Mkuu wa Idara ya ardhi Manispaa ya Ilala Paul Mbembele ambaye alitoa takwimu zisizo sahihi.
Rc Makonda amewataka wananchi wote waliosikilizwa kufika katika ofisi yake Ferbuari 19,mwaka huu kwa lengo la kupatiwa barua zitakazowasaidia kuatiwa wanasheria watakaosimamia kesi zao mpaka watakapo pats haki bila gharama yoyote.
Katika hatua nyingine Rc Makonda amemkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Ilala Salum Hamduni majina ya waliohusika na udalali wa nyumba, wafanyakazi wa benki wanaofanya kazi bila ya kufuata maadili pamoja na wanaogushi kadi za magari na hati za nyumba na kuuza maeneo ya watu, na kumtaka waanze kushughulikiwa Kwanzia leo ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
No comments