KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA
HALMASHAURI ya wilaya ya Kilombero , mkoani Morogoro wamewakatia kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF ) iliyoboreshwa wazee wasiojiweza zaidi ya 7,800 waliopo katika kata 26 ili kuwawezesha kupata huduma bora za matibabu katika vituo vya Afya, Zahanati na hospitali na wategemezi wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo , Dennis Londo alisema hayo mbele ya Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, kabla ya zoezi la ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa baadhi ya wazee wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
Londo alisema kuwa , hadi sasa kiasi cha Sh milioni 13.3 zimetumika kwa ajili ya mpango wa kuwakatia wazee wasiojiweza bima ya afya ya CHF Iliyoboreshwa.
Hata hivyo alisema , halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha wazee wanapatiwa bima ya Afya CHF iliyoboreshwa na lengo ni kuwafikia wazee wasiojiweza zaidi ya 15,000 katika kata zote 26.
“ Halmashauri ya wilaya hii imejipanga vyema na inatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na miongoni mwa mam ohayo ni kundi la wazee wasiojiweza wamenufaka na huduma ya bima ya afya” alisema Londo.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo , David Ligazio aliwataka watendaji wa vituo vya afya, zahanati na hospitali ambaki madirisha ya wazee hayajaanzishwa waanzishe mara moja ili wazee hao wapate unafuu wa huduma kulingana na lengo lililokusudiwa .
Kwa pande wake mkuu wa wilaya ya Kilombero , James Ihunyo alisema , halmashauri hiyo inaendelea kufanya vizuri kutokana na sehemu ya fedha zinazopatikana za makusanyo ya ndani kuelekezwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo kuwakatia bima ya afya wazee wasiojiweza sambamba na kwa halmashauri ya mji Ifakara.
Awali akisoma taarifa ya ugawaji wa kazi hizo , Ofisa Elimu Kata Kalengakelu, Zainab Said alisema, wazee wasiojiweza walionufaika na mpango huo ni wa kutoka kwenye vijiji 23 vya kata ya Chisano, Kalengakelu, Mlimba, Kamwene, Utengule , Masagati na Uchindile .
Akizungumza katika halfa hiyo katibu tawala wa mkoa huo, Tandari alizitaka halmashauri nyingine ndani ya mkoa huo kuiga mfano wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero ili kuhakikisha wazee wote wanakuwa bima ya afya.
Nao baadhi ya wanufaika na mpango huowa CHF iliyoboreshwa ,Nelasi Nyingi na Petro Karubandika kwa nyakati tofauti waliipongeza Serikali na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwa kuwawezesha kuingizwa kunufaika na huduma za afya hasa ikizingatiwa wao wanahauwezo wa kifedha na wategemezi wao.
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa mzee Petro Karubandika mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakati wa zoezi la ugawaji kadi hizo kwa wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba na ( kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa Nelasi Nyingi , mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakati wa zoezi la ugawaji kadi hizo kwa wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba ( kushoto ) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero , Dennis Londo ( kulia) akitoa maelezo mafupi ya mapango wa kuwakatia bima ya afya wazee wasiojiweza kwa Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kutoka kushoto) wakati wa zoezi la ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa wazee wapatao 2,100 wa vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
Baadhi ya wazee wa kata saba za tarafa ya Malimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( hayupo pichani) wakati wa zoezi la ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa wazee wapatao 2,100 wa vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
No comments