CHADEMA TAWI LA KIGOGO FRESH YATOA SAPOTI KWENYE MICHEZO
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
jimbo la Ukonga na ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kata ya Kipunguni,Ally Hassani (kulia) akikabidhi jezi za michezo
jijini Dar es Salaam kwa Meneja wa timu ya mpira wa miguu Super Eagles,Abdallah
Mkoroti ikiwa moja ya utekelezaji wa ahadi ambazo Viongozi wa Tawi la Kigogo Fresh B waliahidi siku zilizopita
walipokabidhi mipira miwili (2).Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) tawi hilo,Jacob Ayo.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Bavicha) tawi la Kigogo fresh B,Abdallah Mlacha(kulia) akikabidhi
jezi za michezo jijini Dar es Salaam kwa Meneja wa timu ya mpira wa miguu Super
Eagles,Abdallah Mkoroti katika uwanja wa Kigogo B relini jijini Dar es Salaam.Wapili
kulia ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Kipunguni,Ally Hassani na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa tawi hilo,Jacob
Ayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
tawi la Kigogo fresh B kata ya Pugu,Jacob Ayo (kulia) akizungumza jambo na
Viongozi pamoja na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Super Eagles katika
hafla ya kukabidhi jezi za michezo iliyofanyika katika kiwanja cha Kigogo B relini
jijini Dar es Salaam.Tukio hilo ni utekelezaji wa ahadi ambayo viongozi wa tawi
hilo waliahidi kwa wachezaji hao siku chache zilizopita baada ya kuwakabidhi
mipira miwili (2).
Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kata ya Kipunguni,Ally Hassani (kulia) akitoa nasaha kwa wachezaji wa
timu ya mpira wa miguu Super Eagles Eagles katika hafla ya kukabidhi jezi za
michezo iliyofanyika katika kiwanja cha Kigogo B relini jijini Dar es Salaam.
Uongozi
wa Kamati tendaji Chama cha Demorasia na Maendeleo Tawi la Kigogofresh B Kata ya Pugu Jimbo la
Ukonga pamoja na Viongozi wa Chama hicho kutoka katika kata nyingine wakiwa katika pozi na Wachezaji wa timu
ya mpira wa miguu Super Eagles huku wakiwa wamevaa jezi ambazo wamekabidhiwa na uongozi huo ikiwa
ni moja ya utekelezaji wa ahadi ambazo waliahidi siku chache zilizopita.
Wachezaji
wa timu
ya mpira wa miguu Super Eagles wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa
wamevaa jezi walizo kabidhiwa na Uongozi wa Kamati tendaji Tawi la Kigogofresh B Kata ya Pugu
Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Wachezaji
wa timu
ya mpira wa miguu Super Eagles wakifanya mazoezi kabla ya mechi ya ligi
inayoendelea katika kata hiyo.
Mchezaji
wa timu
ya Super Eagles,Khalifa Yahaya (kushoto) akichuana vikali na Mchezaji wa Timu
ya Minazini Fc,Ibrahimu Selemani katika mashindano ya ligi inayoendela katika
kata ya Kigogo Fresh jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Timu ya Minazini Fc,Nassoro Mnyelo (kulia)
akimpiga chenga Mchezaji wa timu ya Super Eagles,Rashidi Taji katika mashindano ya ligi inayoendela katika
kata ya Kigogo Fresh jijini Dar es Salaam.
Uongozi
wa Kamati tendaji Chama cha Demorasia na
Maendeleo Tawi la Kigogofresh B Kata ya Pugu Jimbo la ukonga pamoja na Viongozi
wa Chama hicho kutoka katika kata nyingine wakikabidhi kadi za uachama kwa
wakazi wa tawi hilo baada hafla ya kukabidhi jezi za
michezo kwa timu ya mpira wa miguu Super Eagle jijini Dar es Salaam.
Katibu Mwenezi Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kata ya Kipunguni,Ally Hassani akizungumza jambo na wachezaji wa Timu ya Super Eagles.
Katibu Mwenezi Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kata ya
Chanika,Rashidi Simba akizungumza jambo na wachezaji wa Timu ya Super Eagles.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) tawi la Kigogo fresh B kata ya Pugu,Jacob Ayo akitoa nasaha juu ya utunzaji wa jezi walizokabidhi
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Bavicha) tawi la Kigogo fresh B,Abdallah Mlacha(kulia) akizungumza
jambo na Viongozi pamoja na wachezaji wa Timu ya Super Eagles.
No comments