WAITARA APAMBANA NA KERO ZA MAJI JIMBONI
Kaimu
Mhandisi wa Maji Manispaa ya Ilala,Kheri Ally akiwapa maelezo Naibu Waziri wa
maji,Mhe.Jumaa Aweso (watatu kushoto) ,Mbunge wa Jimbo la ukonga Mhe.Mwita
Waitara (kulia) pamoja timu
ya Wahandisi wa maji toka Dawasa, Dawasco, Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri
ya Ilala baada
ya kuwasili katika Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya uzinduzi
wa mradi wa maji uliotekelezwa kwa msaada wa Benki ya dunia.Baada ya uzinduzi
wa mradi huo Waitara aliahidi kutoa shilingi Millioni 10 kutoka kwenye mfuko
wa jimbo hilo kwa ajili ya usambazaji wa maji kutoka kwenye matenki hayo kwenda
kwa wakazi waliopo mbali na mradi huo.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni,Fred Mbenna akizungumza jambo na Viongozi
mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji uliotekelezwa kwa msaada
wa Benki ya dunia uliofanywa na Naibu Waziri wa Maji,Jumaa Aweso pamoja na
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara. Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi za Mh.Waitara kwa
Wananchi wake wa Ukonga kwani baada ya Bunge lililopita aliahidi kuja na Mawaziri
wa Wizara mbalimbali kwa ajili ya utatuzi kero zilizopo jimboni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya llala,Msongela Palela
akizungumza na wakazi wa kata ya Kipunguni (hawapo pichani) katika hafla hiyo.
Katibu Tawala wa Manispaa ya Ilala,Edward
Mpogolo akizungumza na wakazi wa kata ya Kipunguni katika ziara ya Uzinduzi wa
Mradi huo uliopo kata ya hiyo.
Diwani kata ya Kipunguni,Mohamed Msophe akizungumza jambo
katika hafla hiyo.
Katibu Kamati ya Maji wa Mradi wa Kata ya
Kipunguni,Mrighitam Mnzava akisoma taarifa fupi ya mradi huo.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara akizungumza na wakazi wa kata ya Kipunguni
(hawapo pichani) katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kata hiyo uliotekelezwa
kwa msaada wa benki ya dunia uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Waitara aliahidi
kutoa shilingi Millioni 10 kutoka kwenye mfuko wa jimbo hilo kwa ajili ya
usambazaji wa maji kutoka kwenye matenki hayo kwenda kwa wakazi waliopo mbali
na mradi huo.
Naibu
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akizungumza katika uzinduzi huo
Naibu
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akimpa maelekezo Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na
Usambazaji maji,Mhandisi Aron Joseph baada ya kupokea kero za maji zilizopo
kwenye kata ya Kipunguni.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji maji,Mhandisi Aron Joseph akizungumza
jambo na wakazi wa kata ya Kipunguni.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara (kulia) akipeana mikono na Naibu Waziri wa
Maji,Jumaa Aweso katika uzinduzi wa mradi huo.
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kipunguni wakisikiliza kwa
makini hoja zinazoendelea katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kipunguni wakiuliza maswali
kwa Naibu Waziri wa Maji,Jumaa Aweso.
Naibu Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akizungumza jambo na wakazi wa Kata ya Kipunguni baada ya Uzinduzi wa mradi wa maji.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akipeana mikono na wakazi wa Kata ya Kipunguni baada ya Uzinduzi wa mradi wa maji katika kata hiyo.
Kaimu
Mhandisi wa Maji Manispaa ya Ilala,Kheri Ally (kushoto) akiwapa maelezo Naibu
Waziri wa maji,Mhe.Jumaa Aweso (katikati) ,Mbunge wa Jimbo la ukonga Mhe.Mwita
Waitara (watatu kulia) pamoja timu ya Wahandisi wa maji toka Dawasa, Dawasco, Mkoa wa
Dar es Salaam na Halmashauri ya Ilala baada ya kuwasili katika Mradi wa maji Kata ya
Majohe shule ya Msingi Mji Mpya jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya uzinduzi wa
mradi huo uliotekelezwa kwa msaada wa Benki ya dunia.Baada ya uzinduzi wa
miradi huo Waitara aliahidi kutoa shilingi Millioni 10 kutoka kwenye mfuko wa
jimbo hilo kwa ajili ya usambazaji wa maji kutoka kwenye matenki hayo kwenda
kwa wakazi waliopo mbali na mradi huo.
Katibu
wa Mradi wa Maji Majohe,Michael Peter akisoma taarifa fupi ya mradi huo.
Diwani kata ya Majohe,Waziri Mwenevyale akizungumza jambo
katika hafla hiyo.
Katibu Tawala wa Manispaa ya Ilala,Edward Mpogolo
akizungumza na wakazi wa kata ya Majohe katika ziara ya Uzinduzi wa Mradi huo
wa maji uliopo shule ya Msingi Mji Mpya.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara (kulia) akipeana mikono na Naibu Waziri wa
Maji,Jumaa Aweso katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kata Majohe uliotekelezwa
kwa msaada wa benki ya dunia uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Waitara aliahidi
kutoa shilingi Millioni 10 kutoka kwenye mfuko wa jimbo hilo kwa ajili ya
usambazaji wa maji kutoka kwenye matenki hayo kwenda kwa wakazi waliopo mbali
na mradi huo.
Naibu
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akizungumza na wakazi wa majohe katika uzinduzi wa
mradi wa maji wa kata ya hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akimpa maelekezo Mhandisi wa maji Manispaa ya
Ilala,Upendo Lugongo baada ya kupokea kero za maji zilizopo kwenye kata ya
Majohe.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Mji Mpya wakimsikiliza
kwa makini Naibu Waziri wa Maji,Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita
Waitara katika uzinduzi wa mradi huo uliopo shuleni hapo.
Naibu Waziri wa Maji,Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la
Ukonga Mhe.Mwita Waitara wakiwa katika picha ya pamoja Wahandisi
wa maji toka Dawasa, Dawasco, Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri ya Ilala,Wakazi wa kata ya Majohe pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Mji Mpya baada ya uzinduzi wa mradi wa
maji uliopo shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maji mtaa wa Bangulo kata
ya Pugu station,Aloyce Mallya akisoma taarifa fupi ya mradi wa maji wa mtaa huo.
Diwani kata ya Pugu Station,Yohana Ng`ong`a akizungumza
jambo katika hafla hiyo.
Katibu Tawala wa Manispaa ya Ilala,Edward Mpogolo (wapili kushoto) akizungumza na wakazi wa kata ya Pugu station jijini Dar es Salaam leo katika ziara ya Uzinduzi wa Mradi wa maji uliopo katika mtaa wa Bangulo uliotekelezwa na Halmashari ya Ilala.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara akizungumza na wakazi wa kata ya Pugu Station katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kata hiyo uliotekelezwa na Halmashauri ya Ilala uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Waitara aliahidi kutoa shilingi Millioni 10 kutoka kwenye mfuko wa jimbo hilo kwa ajili ya usambazaji wa maji kutoka kwenye matenki hayo kwenda kwa wakazi waliopo mbali na mradi huo.
Naibu
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akizungumza na wakazi wa Bangulo katika uzinduzi wa
mradi wa maji wa kata ya Pugu station jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa jumuia ya watumia maji mtaa wa Bangulo,James Chacha akimueleza jambo Naibu waziri wa Maji,Jumaa Aweso katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Pugu Station wakichangia mada katika uzinduzi huo.
Na
Mwandishi wetu
Mbunge wa jimbo la
Ukonga,Mhe Mwita Waitara amefanya ziara ya uzinduzi wa miradi ya maji akiwa
ameongozana na Naibu Waziri wa maji Mhe.Jumaa Aweso pamoja na timu ya Wahandisi
wa maji toka Dawasa, Dawasco, Mkoa wa Dar es Salaam na wa Halmashauri ya Ilala.
Miradi
iliyozinduliwa leo kupitia ziara hiyo ni
Mradi
wa maji Kata ya Kipunguni ambao ulitekelezwa kwa msaada wa World Bank kwa thamani
ya Shilingi Bilioni 1.3,
Mradi
wa maji Kata ya Majohe Mji Mpya shule ya Msingi ambao nao umetekelezwa
kwa msaada wa World Bank kwa thamani ya Shilingi Milioni 852,
na Mradi
wa maji Kata ya Pugu Station mtaa wa Bangulo ambao ulitekelezwa na Halmashauri
ya Ilala kwa thamani ya Shilingi Milioni 152
Baada ya uzinduzi wa miradi hiyo Waitara aliahidi
kutoa shilingi Millioni 10 kwa kila kata alizotembelea na Naibu Waziri kutoka
kwenye mfuko wa jimbo hilo kwa ajili ya usambazaji wa maji kutoka kwenye
matenki hayo kwenda kwa wakazi waliopo mbali na mradi huo.
Huu
ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi za
Waitara kwa Wananchi wake wa
Ukonga kwani baada ya Bunge lililopita aliahidi kuja na Mawaziri wa Wizara
mbalimbali Jimboni kwa ajili ya kero zilizopo mfano maji, ardhi nk.
No comments