CHADEMA JIMBO LA UKONGA KUSHIRIKI KIKAMILIFU UCHAGUZI WA KINONDONI
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara (kushoto) akisalimiana na Katibu
Wake,Jacob Ayo baada ya Kuwasili katika kata ya Pugu jijini Dar es
Salaam jana kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa jimbo hilo wenye ajenda ya maandalizi ya
kushirikisha Viongozi na wanachama wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) wa jimbo hilo kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi
mdogo wa Mbunge wa jimbo la Kinondoni.Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Ukonga,Lucas Maira.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Ukonga,Lucas Maira (kulia) baada ya
kuwasili katika Mkutano Mkuu wa jimbo wenye ajenda kuhakikisha Viongozi wa
Chama na wanachama wanasapoti Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).Ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafika
Kinondoni siku ya Kupiga kura na baadae kulinda kura mpaka Mgombea wa Chadema
Mhe.Salum mwalimu atangazwe.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mhe Mwita Waitara (kushoto) akisaini kitabu cha mahudhurio
ya Mkutano Mkuu wa jimbo uliofanyika katika kata ya Pugu jijini Dar es
Salaam jana.Katikati Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Ukonga,Lucas Maira na Mwenezi wa Kata ya Kipunguni,Ally Hassani.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Ukonga,Lucas Maira
akizungumza jambo na Viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho katika mkutano
huo.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara
akizungumza na Viongozi pamoja na wanachama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) katika Mkutano Mkuu wa jimbo wenye ajenda kuhakikisha
Viongozi wa Chama na wanachama wanamsapoti Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mhe.salum Mwalimu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkutano huo ulifanyika katika kata ya
Pugu jijini Dar es Salaam jana.Ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafika Kinondoni
siku ya Kupiga kura na baadae kulinda kura mpaka Mgombea wa Chadema Mhe.Salum
mwalimu atangazwe.
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha demokrasia na Maendeleo Jimbo la
Ukonga,Samwel Misalaba akizungumza jambo na Viongozi pamoja na wanachama wa
chama hicho katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ukonga wenye ajenda ya maandalizi
ya kumsapoti mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia Chadema Mhe Salum
Mwalimu.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrsia na Maendeleo (BAWACHA),Doricas
Simburya akizungumza na Viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho katika
mkutano huo.
Katibu
wa Jimbo la Ukonga,Daniel Ruhuro akizungumza katika mkutano.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akimkabidhi
Mwenezi wa Jimbo la Ukonga na Kata ya Kitunda wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo,Nelson Muro bendera za chama hicho.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara
(kulia) akionesha moja ya jezi kwa ajili ya Bonanza la Mpira wa Miguu
WAITARA CUP linalotarajia kuanza baada ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la
Kinondoni.Katikati ni Mwenezi wa Jimbo la Ukonga na Kata ya Kitunda wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo,Nelson Muro na Katibu wa Mbunge,Jacob Ayo.
Baadhi
ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
wakichangia mada katika mkutano.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara
akigawa Vifaa vya Michezo kwa Viongozi wa Chadema kila kata kwa ajili ya
maandalizi ya Mheshimiwa Mbunge liitwalo WAITARA CUP litakalo shirikisha timu 6
kila kata na baadae kupata timu moja ya Jimbola Ukonga.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara akiwa katika picha ya pamoja na Umoja wa
Vijana Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHASO) baada ya kumaliza Mkutano mkuu wa jimbo hilo uliofanyika katika kata ya
Pugu jijini Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mheshimiwa waitara ameongoza
Mkutano Mkuu wa Jimbo lake kwa ajili ya maandalizi ya kushirikisha Viongozi na
wanachama wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Ukonga
kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo
la Kinondoni siku mbili zilizosalia kabla ya siku ya kupiga kura ambayo ni
Jumamosi tarehe 17/02/2018 ni pamoja na kuhakikisha wanafika Kinondoni siku ya
kupiga kura na baadae kulinda kura mpaka mgombea wa Chadema Mhe. Salum Mwalimu
atangazwe
Na baada ya agenda hiyo ya uchaguzi mdogo wa Ubunge
Jimbo la Kinondoni kukamilika Mhe.Waitara aligawa vifaa vya uenezi wa Chadema
kwa Viongozi wa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ukonga
Vile vile Waitara amegawa vifaa vya michezo kwa
Viongozi wa Chadema kila Kata kwa ajili ya maandalizi ya ya Bonanza Mbunge
liitwalo WAITARA CUP litakaloshirikisha timu sita (6) kila Kata na baadae
kupata timu moja ya Jimbo la Ukonga
Vifaa vilivyotayari kwa ajili ya Bonanza hilo
la Mpira wa miguu ni Jezi 518pcs na mipira 60 pamoja na Jezi za Refa na Goli
kipa 26pcs
Bonanza hilo linatarajiwa kuanza baada ya
Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Kinondoni na Siha
Mwisho Mhe.Mbunge wa Ukonga ameahidi kutoa
usafiri wa Makamanda wote wa Ukonga watakaoshiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge
Jimbo la Kinondoni kuanzia kesho na watakao hitaji kwenda wawasiliane na Katibu
Mwenezi wa Jimbo la Ukonga Kamanda Nelson Muro a.k.a Diblo
Namba ya Diblo
Mwenezi wa Jimbo la Ukonga
No comments