WAITARA ALETA NEEMA KWA WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara afanya
ziara Jimboni kwake Ukonga akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Nishati,Subira
Mgalu na Timu ya Wahandisi wa Nishati ya Umeme,Meneja Mkoa wa Pwani Tanesco,Martin
Maduhu,Meneja Mkoa wa Ilala Tanesco,Sotco Nombo,Mkurugenzi wa Huduma za
Ufundi,Wakala wa Nishati Vijijini (REA)Bengel Msophe,Mhandisi Tanesco Gongo la Mboto,Adam
Abdulla,Mhandisi Fred Tweve,Meneja Mradi Pwani,Leo Mwakatobe mna Mwakilishi wa
wizara ya Nishati,Salma Bakari
Lengo la ziara hiyo ni Mradi wa Umeme wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao Mbunge alimuomba Waziri wa Wizara husika
aje azungumze na Wananchi siku ya kuanza utekelezaji mradi huo muhimu jimboni
Maeneo yaliyofikiwa na ugeni huo wa Mhe.Mbunge
na Naibu Waziri wa Nishati ni:-
Kata ya Kivule mtaa wa Bombambili kwa Diwani
wa Kivule Wilson Molel, na Mwenyekiti serikali ya mtaa wa Bombambili,Moses
Marela
Kata ya Msongola mtaa wa Mbondole na mtaa wa
Luhanga kwa Diwani wa Kata ya Msongola Azizi J. Mwalile na Wenyeviti
wa mtaa Mbondole,Thomas Nyamduli na mtaa wa Luhanga,Salum A. Kipendo
Kata ya Zingiziwa mtaa wa Zogoali,Diwani wa
kata hiyo,Hussein Togoro na Mwenyekiti Serikali ya mtaa wa Zogoali,Swalehe Kiloko
Kata ya Chanika,Diwani wa kata hiyo ni Ojambi
Massaburi na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Virobo,Rajabu A. Chuma
Kata ya Buyuni,Diwani wa kata hiyo ni Twaha Malate na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kigezi
Chini,Swalehe A. Swalehe
Ziara hii ni mwendelezo wa jitihada za Mbunge
wa jimbo la Ukonga kutatua kero za wananchi jimboni na pia ni matokeo ya
michango yake Bungeni pamoja na fursa alizopata Bungeni kwa kuuliza maswali na
ujio huu wa Mawaziri Ukonga ndio majibu ya ya maswali hayo.
.............Habari Picha na Ally Hamis............
Mbunge wa Jimbo la
Ukonga, Mwita Waitara (kulia) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakifurahi jambo baada ya
kuwasili katika Kata ya Kivule mtaa wa Bombambili jijini Dar es Salaam jana kwa
ajili ya ziara utatuzi wa kero ya umeme ni pamoja na kutoa taarifa ya Mradi wa
Umeme wa wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao Mbunge alimuomba Waziri wa Wizara
husika aje awape taarifa wananchi siku ya kuanza utekelezaji mradi huo muhimu
kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa
Bombambili,Moses Marela akizungumza na wakazi wa kata Kivule jijini Dar es
Salaam jana katika hafla ya ziara ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
(wapili kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu baada ya kuwasili
katika kata hiyo kwa lengo la kuzungumza na wakazi wa kata hiyo kuhusu mradi wa
Umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao Mbunge alimuomba Waziri aje
awape taarifa siku ya kuanza kwa mradi huo.
Diwani wa kata ya Kivule,Wilson Molel akizungumza
na wakazi wa kata hiyo jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya Mbunge wa
jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (wapili kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Nishati,Subira
Mgalu walipofanya ziara kata hiyo kwa ajili ya utatuzi wa kero za umeme pamoja
na kutoa taarifa ya umeme wa REA ambao Mbunge alimuomba Waziri wa Wizara husika
aje atoe taarifa siku ya kuanza kwa mradi huo pamoja kaisi cha fedha ambacho
kila mkazi atachangia.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
akizungumza na Viongozi pamoja na wakazi wa Kata ya Kivule mtaa wa Bombambili
jijini Dar es Salaam jana katika hafla hiyo ya utoaji wa taarifa ya Umeme wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliofanywa na Naibu Waziri wa Nishati,Subira
Mgalu baada ya kuombwa na Mbunge huyo aje atoe atoe taarifa ya siku ya kuanza
kwa mradi pamoja na kiasi gani kila mwananchi atachangia ili apate huduma hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu akisema
jambo na wakazi wa Kata ya Kivule mtaa wa Bombambili jijini Dar es Salaam jana
katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kivule mtaa wa
Bombambili jijini Dar es Salaam wakiuliza pamoja na kuchangia mada za Mbunge wa
Jimbo la Ukonga ,Mwita Waitara pamoja na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu
(hawapo pichani) baada ya kuwasili katika kata hiyo jijini Dar es Salaam jana
kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero ya umeme pamoja na kutoa taarifa ya
umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Meneja wa Tanesco mkoa wa Ilala,Sotco Nombo
akizungumza na wakazi wa Kata ya Kivule mtaa wa Bombambili jijini Dar es Salaam
jana baada ya kuulizwa swali na wakazi kutokana na kero za ukosefu wa umeme
katika kata hiyo.Kulia ni Mhandisi Tanesco Gongo la Mboto,Adam Abdulla.
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kivule mtaa wa
Bombambili wakisikilza kwa makini mada zitolewazo na ugeni huo.
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu (kulia)
akipeana mikono na wakazi wa Kata ya Kivule mtaa wa Bombambili jijini Dar es
Salaam baada ya kumaliza ziara katika kata hiyo na kuelekea katika kata nyingine
za Jimbo la Ukonga zenye kero kama hiyo ya Ukosefu wa Umeme.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
(kushoto),Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu na Mwenyekiti wa Serikali ya
mtaa wa Bombambili,Moses Marela,wakiongozana pamoja kuelekea katika kisima cha
Shule ya Msingi Bomba Mbili ambacho kipo tayari lakini kina tatizo la kukosa
umeme ambalo lina kwamisha huduma muhimu ya maji kwa Wanafunzi wa Shule hiyo
kuwa shida na kusababisha wanafunzi kwenda kuomba maji kwa wakazi walio jirani
na Shule hiyo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Mbondole,Thomas Nyamduli akizungumza jambo na wakazi wa kata ya Msongola jijini
Dar es Salaam jana katika hafla ya Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
(watatu kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu (watatu kulia)
kuwasili katika kata hiyo kwa ajili ya kutatua kero ya ukosefu wa umeme katika
kata hiyo ni pamoja na kutoa taarifa ya mradi wa umeme wa Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) ambapo Mbunge alimuomba Waziri wa Wizara husika aje katika jimbo
atoe taarifa pamoja na kutaja bei ya mradi huo kwa mwananchi atakaye hitaji
huduma hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
akizungumza na Viongozi pamoja na wakazi wa Mtaa wa Mbondole kata ya Msongola
jijini Dar es Salaam jana katika hafla
ya ziara ya utaoji wa taarifa ya Umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
uliofanywa na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu baada ya kuomba na Mbunge
huyo aje atoe atoe taarifa ya siku ya kuanza kwa mradi pamoja na kiasi gani
kila mwananchi atachangia ili apate huduma hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu akisema
jambo na wakazi wa Mtaa wa Mbondole kata ya Msongola jijini Dar es Salaam jana katika hafla hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Mbondole kata ya
Msongola wakisikilza kwa makini mada zitolewazo na ugeni huo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
(katikati) akipeana mikono na wakazi wa Mtaa wa Mbondole kata ya Msongola jijini
Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake katika mtaa huo na kuelekea katika
kata nyingine za Jimbo la Ukonga zenye kero kama hiyo ya Ukosefu wa Umeme.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Luhanga kata
ya Msongola,Salum Kipendo akimkaribisha Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
(wapili kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu baada ya kuwasili
katika kata hiyo kwa ajili ya ziara ya kusikiliza kero za umeme pamoja na kutoa
taarifa ya Umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Luhanga kata ya
Msongola wakisikilza kwa makini mada zitolewazo na ugeni huo.
Diwani kata ya Msongola,Azizi Mwalile
akizungumza jambo na wakazi wa Mtaa wa Luhanga katika ziara ya Mbunge wa Jimbo
la Ukonga pamoja na Naibu Waziri wa Nishati iliyofanyika katika shule ya Msingi
Kiboga yenye agenda ya kusikiliza kero za ukosefu wa umeme pamoja na kutoa taarifa ya mradi
wa umeme wa REA kuanza lini.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akisema
jambo na wakazi wa Mtaa wa Luhanga kata ya Msongola jijini Dar es Salaam jana katika hafla hiyo.
Naibu waziri wa Nishati,Subira Mgalu akisema
jambo na wakazi wa Mtaa wa Luhanga kata ya Msongola jijini Dar es Salaam jana katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Luhanga kata
ya Msongola Dar es Salaam wakiuliza maswali pamoja na kuchangia mada za Mbunge wa Jimbo
la Ukonga ,Mwita Waitara pamoja na Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu (hawapo
pichani) baada ya kuwasili katika kata hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili
ya kusikiliza na kutatua kero ya umeme pamoja na kutoa taarifa ya umeme wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Zogoali kata ya Zingiziwa wakisikilza kwa makini mada zitolewazo na ugeni huo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akizungumza jambo na wakazi wa mtaa wa Zogoali kata ya Zingiziwa.
Naibu waziri wa Nishati,Subira Mgalu nae alizungumza katika ziara hiyo mtaa wa Zogoali kata ya Zingiziwa.
Wakazi wa mtaa wa Zogoali kata ya Zingiziwa
wakiuliza maswali katika ziara hiyo.
Baadhi wakazi wa mtaa wa Virobo kata ya Chanika wakisikilza kwa makini agenda inayojadiliwa na ugeni huo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
akizungumza jambo na wakazi wa mtaa wa Virobo kata ya Chanika.
Wakazi wa kata ya Chanika wakiuliza maswali katika ziara
hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu (kulia) akipeana mikono na wakazi wa Kata ya Buyuni jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katikia kata hiyo kwa ajili ya ziara yake pamoja na Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara yenye agenda ya Mradi wa Umeme wa REA ambao Mbunge alimuomba Waziri wa Wizara husika aje kutoa taarifa kwa wananchi siku ya kuanza utekelezaji mradi huo muhimu kwa wananchi wa jimbo hilo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Buyuni wakisikiliza kwa makini hoja za Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati baada a kuwasili katika kata hiyo.
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Buyuni Dar es Salaam wakiuliza maswali kwa Wahandisi wa Tanesco,Mkurugenzi wa REA na Mwakilishi wa Wizara ya Nishati.
Meneja wa Tanesco mkoa wa Pwani,Martini Maduhu
akijibu maswali ya Wakazi wa kata ya Buyuni.
No comments