WAITARA MGUU KWA MGUU NA NAIBU WAZIRI MPAKA JIMBONI
Mbunge wa
Jimbo la Ukonga,Mhe Mwita Waitara (kushoto) akimtambulisha Naibu Waziri wa Mazingira Mhe.Kange Lugola (wapili kushoto) kwa Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa Mwanagati kata ya Mzinga,Chacha Momba baada ya kuwasili katika kata hiyo
kwa ajili kutatua kero ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na Mwekezaji aliyejenga
Kiwanda cha Kuyeyusha Taka,Nestling
Company Limited katika makazi ya Wananchi kinyume na Sheria za Wizara husika.Waitara
alilazimika kuja na Naibu Waziri Lugola kutoka Dodoma baada ya kupokea malalamiko
ya muda mrefu kuhusu kiwanda hicho toka kwa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa
Mwanagati,Ofisi ya Diwani pamoja na wananchi waishio mtaa wa Mwanagati Block 5
na 6 kilipo kiwanda hicho.Kushoto ni Diwani Viti maalumu Manispaa ya Ilala,Sara
Katanga.
Mbunge wa
Jimbo la Ukonga,Mhe Mwita Waitara (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha
Kuyeyusha Takataka,Nestling Company Limited,Athumani Hamisi baada ya kuwasili
kiwandani hapo na Naibu Waziri wa Mazingira Mhe.Kange Lugola (wapili kulia) kwa aijli ya kutatua kero ya
uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na kiwanda hicho kilichopo karibu na makazi
wa wananchi wa Mtaa wa Mwanagati kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo.
Mwekezaji wa
Kiwanda ya Kuyeyusha Takataka,Nastling Company Limited,Michael Makenge (kulia) akizungumza
jambo na Naibu Waziri wa Mazingira, Mhe.Kange Lugola (katikati) baada ya kuwasili
kiwandani hapo ka aijili ya kutatua kero ya uchafuzi wa mazingira inayofanywa
na kiwanda hicho kilichopo karibu na makazi na wananchi wa Mwanagati jijini Dar
es Salaam leo.Wapili Kushoto ni Diwani kata ya Mzinga,Job Isaack na Mbunge wa
Jimbo la Ukonga,Mhe Mwita Waitara.
Naibu Waziri
wa Mazingira,Mhe.Kange Lugola (watatu kushoto) akimueleza jambo Mwekezaji wa
Kiwanda ya Kuyeyusha Takataka,Nastling Company Limited,Michael Makenge (kulia) malalamiko
ya muda mrefu aliyopokea kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mwanagati,Ofisi ya
Diwani pamoja na Wakazi walio karibu na kiwanda hicho jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu wa
Mazingira Kanda ya Mashariki (NEMC) Jaffar Chimgeye (kulia) akimsomea Naibu
Waziri wa Mazingira,Kange Lugola (watatu kushoto) barua waliyomtumia Mwekezaji
wa Kiwanda cha Kuyeyusha takataka,Nestling Company Limited barua ya kuacha
shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho.
Inspekta Gwamaka akimfunga pingu Mwekezaji wa Kiwanda cha Kuyeyusha Takataka
Naibu
Waziri wa Mazingira,Mhe.Kange Lugola (kulia) akimueleza jambo Inspekta Gwamaka
(kushoto) katika ziara ya kutatua kero ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa
na Kiwanda cha Kuyeyusha takataka,Nestling Company Limited kilichopo karibu na
makazi wa wananchi wa Mtaa wa Mwanagati kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam
leo. Wapili Kulia ni Diwani kata ya Mzinga,Job Isaack na Mbunge wa Jimbo la
Ukonga,Mhe Mwita Waitara.
Mbunge wa
Jimbo la Ukonga,Mhe Mwita Waitara (katikati) akizungumza jambo katika ziara
hiyo.
Mkazi wa
Mtaa wa Mwanagati kata ya Mzinga,Saimon Nguka (wapili kushoto) akichangia hoja
katika ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira Mhe.Kange Lugola (kulia) ya kutatua
kero ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na Kiwanda cha Kuyeyusha
takataka,Nestling Company Limited kilichopo karibu na makazi wa wananchi wa
Mtaa wa Mwanagati kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo.
Diwani kata
ya Mzinga,Job Isaack (wapili kulia) akizungumza jambo katika ziara hiyo.
Mkazi wa
Mwanagati kata ya Mzinga,Jofrey Erneo (katikati) akitoa shukrani zake za dhati
kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara pamoja Naibu Waziri wa
Mazingira,Mhe.Kange Lugola baada ya kuwasili Katika kata hiyo kwa ajili ya
kutatua kero za Uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na Kiwanda cha Kuyeyusha
takataka,Nestling Company Limited kilichopo karibu na makazi wa wananchi wa
Mtaa huo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Miundombinu Mtaa wa Mwanagati Brighton Chiza akimueleza jambo
Naibu Waziri.
Mbunge wa
Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akizungumza na Wakazi wa Mwanagati
jijini Dar es Salaam leo katika ziara ya
kutatua kero ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na Kiwanda cha Kuyeyusha
takataka,Nestling Company Limited kilichopo karibu na makazi wa wananchi wa
Mtaa huo.
Mkazi wa
Mwanagati Block 6,Odilia Chonya akiuliza swali katika hafla .
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Mwanagati,Chacha Momba akizungumza na wakazi wa mtaa huo
jijini Dar es Salaam leo katika ziara ya Naibu waziri wa Mazingira,Mhe.Kange
Lugola (hayupo pichani) alipotembelea mtaani kwa ajili ya kutatua kero za
Uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na Kiwanda cha Kuyeyusha takataka,Nestling
Company Limited kilichopo karibu na makazi wa wananchi wa Mtaa huo jijini Dar
es Salaam leo.
Diwani wa
Kata ya Mzinga,Job Isaack akizungumza jambo.
Mkazi wa
Mzinga,Ibrahimu Kitege akiuliza swali katika hafla hiyo.
No comments