BALOZI WA UJERUMANI TANZANIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA WAHANGA UTAWALA WA HITLER
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani. Kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter. |
BALOZI wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter ameshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, yalioshirikisha wanafunzi mbalimbali wa Shule za Sekondari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo aliwataka vijana kujitambua, kupenda kujifunza historia na pia kutokubali kutumika kuchochea vurugu katika maeneo yao.
Maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa mfumo wa 'Nazism' uliolenga kuwateketeza Wayahudi kwa kuamini si binadamu bora yalipoteza uhai wa watu takribani milioni sita wakiwemo watoto. Mfumo ambao pia ulitokomeza watu wenye ulemavu na wafupi kwa kuangamizwa kwa kutumia gesi za sumu na pamoja na moto.
Aidha alisema baadhi ya maeneo vijana wanaweza kujikuta wanatumika katika matukio yanayochangia vurugu hivyo kuna kila sababu ya wao kupewa elimu ya kujua historia kwa undani ili wasiweze kutumika kwa namna yoyote.
"Upo umuhimu wa vijana kutokubali kushiriki katika masuala ya ukatili, vurugu za aina yoyote ile...alisema vijana wanapaswa kujitambua na kufahamu historia na jukumu lao la kulinda amani kwa faida ya mataifa yao,"
Vijana hao kutoka shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam walipata elimu pia kutoka kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter juu ya historia ya mauaji hayo, ambapo walipata fursa za kujadili na kuuliza maswali tofauti kutoka kwa balozi huyo raia wa Ujerumani.
No comments