Breaking News

WANACHAMA WA CHADEMA KATA YA CHANIKA WAPATA NEEMA YA OFISI

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Mwita Waitara (wapili kulia) akizungumza na viongozi wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ngazi ya Kata katika hafla ya kukabidhiwa ofisi ya chama hicho kutoka kwa familia ya Bwana na Bibi Charles Sangiwa jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Katibu wa Chama Kata ya Chanika, Charles Sangiwa na Mkewe. . Waitara aliahidi kuchangia viti kumi (10) vya ofisi pamoja na meza moja (1) kwa ajili ya matumizi ya ofisi hiyo mpya.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Mwita Waitara (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama pamoja na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kata ya Chanika katika hafla ya kukabidhiwa ofisi ya Chama hicho na familia ya Bwana na Bibi Charles Sangiwa jijini Dar es Salaam jana.Kutoka kushoto ni Kushoto ni Katibu wa Chama Kata ya Chanika, Charles Sangiwa na Mkewe.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Mwita Waitara akizungumza wanachama pamoja na viongozi wa Chadema ngazi ya Kata Nyumbani kwa Bwana Sangiwa katika hafla ya kukabidhiwa ofisi ya chama hicho kutoka kwa familia ya Bwana na Bibi Charles Sangiwa jijini Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Mwita Waitara Sikukuu ya Christmas ya jana alialikwa Chanika na viongozi wa Chadema ngazi ya Kata wakiongozwa na Katibu wa Chama hicho Kata ya Chanika, Charles Sangiwa 

Sherehe ya mwaliko huo wa Mhe. Waitara Chanika ilifanyika nyumbani kwa Sangiwa na baadae Waitara alizindua ofisi ya Chadema ngazi ya Kata ambayo ilitolewa bure na Bwana na Bibi  Sangiwa kwa matumizi ya shughuli za Chama muda na saa zote bila malipo

Mhe. Waitara kwa niaba ya Chadema aliishukuru Sana familia ya  Charles Sangiwa kwa imani kubwa walioonyesha kwa Chama Kata na Jimbo kwa pamoja 

Baada ya uzinduzi huo Mhe. Waitara  aliahidi kuchangia viti kumi (10) vya ofisi pamoja na meza moja (1) kwa ajili ya matumizi ya ofisi hiyo mpya  

Vilevile Mhe. Waitara aliweza kutoa papo hapo bendera ishirini  (20) na Skafu kumi (10) 

Pia Mhe. Mbunge aliwashukuru baadhi ya wazee wa Kata ya Chanika hasa mtaa wa Tungini kwa kukubali kwao kutoa bure maeneo yao kwa ajili ya viwanja vya michezo, na maeneo hayo wazee hao waliyakabidhi kwa viongozi wa Chadema Kata ya Chanika miezi miwili iliyopita 

Mhe. Waitara alishauri ni vema uzalendo ulioonyeshwa na Katibu wa Chadema Chanika ukaigwa kwenye Kata nyingine ndani ya Jimbo la Ukonga. 

No comments