WAITARA ALETA NEEMA KWA WAJASIRIAMALI WA JIMBO LA UKONGA
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mh.Mwita
Waitara (wapili kulia) akizungumza na wakazi wa kata ya Kivule jijini Dar es
Salaam jana katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama
wafanyabiashara ndogondogo.Mafunzo hayo yamezinduliwa rasmi katika kata ya
Kivule na kuendelea katika kata nyingine zilizobakia za jimbo la Ukonga.Kutoka
kulia ni Afisa Maendeleo wa Kata ya Kivule,Anna Masawe.
Afisa Maendeleo wa Kata ya Kivule,Anna
Masawe akizungumza na wakazi wa Kivule katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya
ujasiriamali kwa akina mama wafanyabiashara wadogowadogo yaliyofanyika Kivule jijini
Dar es Salaam jana.Wapili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe Mwita
Waitara,Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Yangeyange kata ya Msongola,Mwita Mahando
na Meneja Mafunzo ya Ujasiria mali wa Kampuni ya Elnet Africa,Musa Ndile.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji
na Kuhifadhi mazao ya kilimo (TFPC),Idd Mkolamasa akiwaonyesha wakazi wa Kivule
mashine za kisasa ya kusindika Nyanya katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali
kwa akina mama wafanyabiashara wadogowadogo yaliyofanyika Kivule jijini Dar es Salaam
jana.Mafunzo hayo yameanza kutolewa katika Kata ya Kivule baada ya kufunguliwa
na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara na yataendelea kwa kata
zilizobakia za jimbo hilo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji na
Kuhifadhi mazao ya kilimo (TFPC),Idd Mkolamasa akiwaonyesha wakazi wa Kivule mashine
za kisasa ya kusaga nyama pamoja na kutengeneza soseji katika hafla ya ufunguzi
wa mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama wafanyabiashara wadogowadogo yaliyofanyika
Kivule jijini Dar es Salaam jana.
Mke wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji na Kuhifadhi mazao ya kilimo (TFPC),Mwami
Makaranga akiwaonesha akinamama wajasiriamali wadogowadogo mashine ya kisasa
kukamulia juisi ya miwa katika hafla ya
ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali yalifanyika katika kata ya Kivule jijini
Dar es Salaam jana.
Afisa Maendeleo wa Kata ya Kivule,Anna Masawe (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mh.Mwita Waitara katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa akinamama wafanyabiashara ndogondogo uliofanyika katika kata ya Kivule jijini Dar es Salaam jana.Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Yangeyange kata ya Msongola,Mwita Mahando.
Mkazi wa Kata ya Msongola,Mwing'a Machiba
akiuliza swali kwa wakufunzi wa ujasiriamali katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo
hayo iliyofanyika katika kata ya kivule jijini Dar es Salaam jana.
Diwani wa Kata ya Kivule,Wilson Moses (kulia) akizungumza na akinamama wajasiriamali wadogowadogo katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali yalifanyika katika kata hiyo jijini Dar es Salaam jana.Mafunzo hayo yameanza kutolewa katika kata ya kivule na yatatolewa kwa kata nyingine zilizosalia za jimbo la Ukonga.Wapili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe Mwita Waitara,Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Yangeyange kata ya Msongola,Mwita Mahando na Meneja Mafunzo ya Ujasiria mali wa Kampuni ya Elnet Africa,Musa Ndile.
Baadhi ya akinamama wajasiriamali wakisikiliza kwa makini mada zitolewazo wa wakufunzi wa ujasiriamali walioletwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo iliyofanyika Kivule jijini Dar ea Salaam jana.
Mwalimu wa Vicoba endelevu,Sifa Maneno akionyesha akina mama wa kata ya Kivule jinsi ya kutengeneza batiki katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika kata hiyo jijini Dar es Salaam jana.Ufunguzi wa Mafunzo hayo ulifanywa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara na mafunzo hayo yalianza hapohapo baada ya kufunguliwa na yataendelea kutolewa kwa kata zilizosalia.
Baadhi ya akinamama wajasiriamali wakisikiliza kwa makini mada zitolewazo wa wakufunzi wa ujasiriamali walioletwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo iliyofanyika Kivule jijini Dar ea Salaam jana.
Mwalimu wa Vicoba endelevu,Sifa Maneno akionyesha akina mama wa kata ya Kivule jinsi ya kutengeneza batiki katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika kata hiyo jijini Dar es Salaam jana.Ufunguzi wa Mafunzo hayo ulifanywa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe. Mwita Waitara na mafunzo hayo yalianza hapohapo baada ya kufunguliwa na yataendelea kutolewa kwa kata zilizosalia.
No comments