WAITARA AZUNGUMZA NA WAKAZI WA KATA YA UKONGA
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mh.Mwita Waitara akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa Kata ya Ukonga katika mkutano uliokuwa na agenda ya kuwasilisha kwa wakazi hao miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Halmashauri ya Ilala pamoja na mfuko wa jimbo kupitia uwakilishi wa mbunge kwa wananchi wa Ukonga.Mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Transfoma karibu na mazizini jijini Dar es Salaam leo.
Diwani kata ya Ukonga,Jumaa Mwipopo akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa Kata hiyo katika mkutano uliokuwa na agenda ya kuwasilisha kwa wakazi hao miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Halmashauri ya Ilala pamoja na mfuko wa jimbo kupitia uwakilishi wa mbunge kwa wananchi wa Ukonga.Mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Transfoma karibu na mazizini jijini Dar es Salaam leo.
Mweka Hazina wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,Gaston Makweta akichangia mada katika
mkutano wa kuwasilisha miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Halmashauri ya Ilala pamoja na mfuko wa jimbo kupitia uwakilishi wa mbunge kwa wananchi wa Ukonga
uliofanyika katika viwanja vya Transfoma karibu na mazizini jijini Dar es
Salaam leo.
Mkazi wa Kata ya Ukonga,Ramadhani Mchechu akiuliza swali katika
mkutano wa kuwasilisha miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Halmashauri ya Ilala pamoja na mfuko wa jimbo kupitia uwakilishi wa mbunge kwa wananchi wa Ukonga
uliofanyika katika viwanja vya vya Transfoma karibu na mazizini jijini Dar es
Salaam leo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Ukonga wakisikiliza kwa
makini mada zitolewazo na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara na Diwani
wa kata hiyo,Jumaa Mwipopo (hawapo pichani) katika mkutano wa kuwasilisha
miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Halmashauri ya Ilala pamoja na mfuko wa jimbo
kupitia uwakilishi wa mbunge kwa wananchi wa Ukonga uliofanyika katika viwanja
vya vya Transfoma karibu na mazizini jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mh.Mwita Waitara (kulia)
akipeana mikono na wakazi wa kata ya Ukonga katika mkutano wa kuwasilisha
miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Halmashauri ya Ilala pamoja na mfuko wa jimbo
kupitia uwakilishi wa mbunge kwa wananchi wa Ukonga uliofanyika katika viwanja
vya vya Transfoma karibu na mazizini jijini Dar es Salaam leo.
Na mwandishi wetu
Mbunge wa jimbo la
Ukonga Mhe. Mwita Waitara leo amefanya
Mkutano wa hadhara katika Kata ya Ukonga mtaa wa Mazizini akiwa ameongozana na Diwani
wa Kata ya Ukonga Mhe.Jumaa Mwipopo
Agenda kuu ilikuwa ni
kuwasilisha kwa wakazi miradi mbali-mbali iliyotekelezwa na Halmashauri ya Ilala pamoja na mfuko
wa Jimbo kupitia uwakilishi wa Mbunge kwa
wananchi wa Jimbo la Ukonga
Miongoni mwa miradi
iliyotekelezwa ndani ya Kata mbalimbali kati ya Kata 13 za Jimbo la Ukonga ni
uchimbaji wa visima vya maji, Ujenzi wa Shule mpya, Vituo vya afya, Zahanati,
barabara, ujenzi wa vituo vya polisi pmaoja na vivuko.
Vile vile Mhe. Waitara
amepokea kero mbalimbali toka kwa wananchi na ameahidi kuzifanyia kazi kwa
kushirikiana na viongozi wa mamlaka zinazohusika Serikalini.
No comments