TMRC KWA HILI MUNGU ANAWAONA
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifedha
inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya (kushoto) akipeana mikono na Mlezi Mkuu
wa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa
baada ya kuwasili kituoni hapo kwa ajili ya kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas
zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Mkurugenzi
wa Fedha wa Kampuni hiyo Oswald Urassa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifedha
inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya (kushoto) akipeana mikono na Msajili wa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani
Orphanage Centre,Joseph Mwakisyala baada ya kuwasili kituoni hapo kwa ajili ya
kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili
shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Mlezi Mkuu wa Kituo
hicho,Elias Mwakalukwa.
Afisa Utawala wa Kampuni ya Kifedha
inayokopesha Mabenki (TMRC),Elizabeth Lyakurwa (kushoto) akipeana mikono na
Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias
Mwakalukwa katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani
ya Shilingi Milioni Mbili shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Meneja
Rasilimali watu wa Kampuni hiyo,Olympia Nangela.
Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulea watoto
yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa(kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kifedha inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya wakati wa hafla
ya kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili
iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi
wa fedha wa Kampuni hiyo,Oswald Urassa.
Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulea watoto
yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa akiwaombea Vingozi wa Kampuni
ya Kifedha inayokopesha Mabenki (TMRC) pamoja na walimu wa Kituo hicho katika
hafla ya kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni
Mbili iliyofayika shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.
Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulea watoto
yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa(kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (hawapo pichani) wakati wa hafla
ya kukabidhiwa zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili
kutoka kwa Kampuni ya Kifedha inayokopesha Mabenki (TMRC) iliyofanyika shuleni
hapo.Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni
hiyo Oscar Mgaya, Meneja Rasilimali watu,Olympia Nangela, Mkurugenzi wa
fedha Oswald Urassa na Afisa Utawala,Elizabeth Lyakurwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifedha
inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (hawapo pichani) wakati wa hafla
ya kukabidhi msaada wa vyakula pamoja na mahitaji muhimu yenye thamani ya
shilingi Milion 2 kwa Kituo cha kulea
watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre.Kutoka kushoto ni Mlezi Mkuu wa Kituo
cha kulea watoto Elias Mwakalukwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifedha
inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akikabidhi zawadi ya Sikukuu
ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili kwa mwakilishi wa Wanafunzi
wa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre jijini Dar es Salaam
leo.Kutoka kulia ni Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulea watoto yatima,Elias Mwakalukwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifedha
inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akikabidhi msaada wa
vyakula pamoja na mahitaji muhimu vyenye thamani ya Shilingi Milion 2 kwa Mlezi
Mkuu wa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa
jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto ni Mkurugenza wa Fedha wa Kampuni hiyo,
Oswald Urassa.
Wanafunzi wa Kituo cha kulea watoto
yatima Kiwalani Orphanage Centre wakisikiliza kwa makini mada zitolewazo na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifedha inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya(hayupo
pichani) katika hafla ya kukabidhiwa zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani
ya Shilingi Milioni Mbili iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifedha
inayokopesha Mabenki (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akizungumza na
wanafunzi pamoja na walimu wa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage
Centre (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye
thamani ya Shilingi Milioni Mbili iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es
Salaam leo.
Mwanafunzi wa Kituo cha kulea watoto
yatima Kiwalani Orphanage Centre,Izack William akitoa shukrani kwa Viongozi
kutoka Kampuni ya Kifedha inayokopesha Mabenki (TMRC) katika hafla ya
kukabidhiwa zawadi ya Sikukuu ya Krismas
zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es
Salaam leo.
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya Kifedha inayokopesha Mabenki (TMRC) imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya
Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) kwa Kituo cha Watoto yatima cha Kiwalani
(Kiwalani Orphanage Centre) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Zawadi
hizo zimekabidhiwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bw. Oscar P. Mgaya kwa
Mlezi Mkuu wa Kituo hicho, Mchungaji Elias Mwakalukwa,katika ghafla iliyofanyika
kwenye Kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa zawadi zilizotolewa
kwa kituo hicho cha watoto yatima ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, unga wa
sembe, maharage ,sabuni za kufulia na kuogea, sukari,chumvi, dawa za meno, majani ya chai,kalamu na madaftari
“Kwa upendo wetu wadhati kabisa tumeona umuhimu wakushiriki
pamoja na watoto yatima, ambao wapo katika mazingira magumu,
katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas mwaka 2017,” alisema Bw. Mgaya.
Bw.
Mgaya, alisema kuwa taasisi yake imeamua kujumuika na watoto hawa yatima katika
kuelekea kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa kutoa zawadi mbalimbali za vyakula
kama njia ya kuwafanya wajisikie furaha.
Hata
hivyo, Mtendaji Mkuu huyo, amezitaka taasisi nyingine na watu binafsi kujitoa kwa
dhati kuwasaidia watoto walioko maeneo mbalimbali nchini.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Kituohicho, Mchungaji Elias Mwakalukwa, ameishukuru TMRC, kwa msaada
huo na ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano wao.
“Tunaishukuru
sana TMRC, ninyi mmeonyesha mfano na hakika mmeonyesha upendo wa dhati kwa watoto
hawa. Niziomba taasisi nyingine kuchukua mfano huu uliofanywa na taasisi yenu,”
Mchungaji Elias Mwakalukwa alisema.
Aliongeza
kuwa uhitaji wa misaada kwa kituo chake ni mkubwa, lakini taasisi yao inapata faraja
kupata wadau wanaoona umuhimu wa kusaidia watoto hao yatima.
No comments