Breaking News

WAITARA AALIKWA KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA WANAWAKE


Na mwandishi wetu
Hivi Karibuni  Uongozi wa Jukwaa la wanawake mtaa wa Bombani Kata ya Pugu wamefika ofisini kwa Mbunge wa jimbo la Ukonga Mhe.Mwita Waitara  kumuomba ashiriki kwenye Uzinduzi wa  Jukwaa lao (Umoja) lenye jumla ya wamama wapatao mia nne (400) 

Pia Uongozi wa Jukwaa hilo la wanawake  wamemuomba Mhe. Waitara awawezeshe vifaa vya uzinduzi wa Umoja wao Mfano Viti, Matent, na Mziki.

Ni mwendelezo wa Wananchi wapiga kura wa Mhe. Waitara kufika ofisini kumpongeza kutokana na jinsi anavyowawakilisha vyema Bungeni na Jimboni pia.

Wananchi hao walifika ofisini kwa  wao wakiwa wameongozana na Mwenyekiti  wa Serikali ya mtaa wa Pugu-Bombani Gido Lupiana.

Uzinduzi huo wa Jukwaa la Wanawake wa Pugu Bombani ni utafanyika 14 February 2018.


No comments