WASHINDI WA DROO YA PILI MLIMANI CITY WAPATIKANA
Mratibu
wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping fest),
Neema Utouh akichanganya kuponi ili kupata washindi 20 wa droo ya pili wa vocha
ya thamani ya Shilingi 100,000 kila mmoja ya kufanya manunuzi tena katika duka
lolote ndani ya Mlimani City iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City Dar es
Salaam.Wengine ni mabalozi wa Promosheni hiyo.
Mratibu
wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping fest),
Neema Utouh(kushoto) akimkabidhi vocha ya thamani ya Shilingi 100,000, Grace
Mushi mara baada ya kuibuka mshindi katika droo ya pili ya promosheni ya fanya
manunuzi Mlimani City na ushinde(Mlimani City Grand Shopping Fest) iliyofanyika
Mlimani City mwishoni mwa wiki.
Mratibu
wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping fest),
Neema Utouh akifungua kuponi ya msindi wa kwanza wa droo ya pili wa vocha ya
thamani ya Shilingi 100,000 ya kufanya manunuzi tena katika duka lolote ndani
ya Mlimani City iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City Dar es
Salaam.Wengine ni mabalozi wa Promosheni hiyo.
Na Mwandishi wetu
WASHINDI
20 wa promosheni ya Mlimani City Shoping Fest wamepatika mara baada ya kucheza
droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City jijini Dar es Salaam ambao ni
Grace Mushi,Samson K. Samson,Grace Hoka, Mnyamani, Mushi Kimaro, Judith Shayo,
Erick Msumati, Gwamaka Hezron, Ally Nyaga, Amani Sepetu, Masood Wanani,
Jonathan Nkya, Hellen Mngutu, Omary Khary, Linda Bahati, Agrum Maringo, Saidi
Kheri, Paul Charles, Beatrice Kaswaga na Suzan Said.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa
Kampeni hiyo, Neema Utouh alisema mpaka sasa jumla ya washindi 40 wamepatikana
tangu Kampeni hiyo izinduliwe rasmi na tayari zawadi zao za vocha ya kufanya
manunuzi yenye thamani ya Shilingi 100,000 kila mmoja wameshapatiwa.
Alisema Neema, ni nafasi yakow ewe ambaye
hujaja kufanya manunuzi mlimani City karibia fanya manunuzi ya shilingi laki
moja au zaidi utapewa kuponi ambayo itakuwezesha kuingia moja kwa moja kwenye
droo ya ushindani.
Hii ni wiki ya pili taku promosheni hii
izinduliwe na bado wiki tatu ambapo mwisho kabisa kutakuwa na droo kubwa ambayo
mshindi mmoja atajishindia vocha yenye thamani ya shilingi 10,000 000 ambayo
itamuwezesha kufanya manunuzi duka lolote ndani ya Mlimani City pamoja na
washindi watano watakaojishindia vocha yenye thamani ya shilingi milioni moja
kila mmoja.
Mwisho Neema alitoa wito kwa wateja wa mlimani
City na watu wote kujitokeza kwa wingi kuja kufanya manunuzi Mlimani City
katika kipindi hiki cha siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya ili kupata fursa ya
kushiriki katika shindano la promosheni ya “Mlimani City Shopping Fest”.
AKatika kusherehekea Sikukuu za X-Mas na Mwaka
Mpya, uongozi wa Mlimani City kwa kushirikiana na wafanyabiashara wenye maduka
ndani yake umetangaza ofa maalumu kwa wateja wake watakaofanya manunuzi
katika msimu huu wa sikukuu.
Ofa hiyo inatoa fursa ya kujishindia zawadi
mbalimbali ambazo zimegawanywa kwa makundi matano ambapo kila wiki washindi 20
watajishindia vocha yenye thamani ya kufanya shoping kwa vitu vya thamani ya
Shilingi 100,000 lakini pia watakuwa mwameingia moja kwa moja kwenye droo kubwa
ya mwisho ambayo mshindi wa kwanza atajishindia vocha ya manunuzi ya bidhaa za
nyumbani yenye thamani ya Shilingi Milioni 10, na mshindi 5 watajinyakulia
vocha yenye thamani ya shilingi milioni 1, kila mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Meneja mkuu wa Mlimani City Ndugu Pastory Mrosso alisema kuwa
washindi wa kila wiki watafanya manunuzi katika duka lolote ndani ya Mlimani
City kwa kutumia vocha zao.
Promosheni hii maalumu imeanza Desemba 15 na
inatarajia kufikia mwisho Januari 14, 2018, ambapo droo kubwa ya kupata mshindi
wa kwanza wa Vocha yenye thamani ya Shilingi milioni 10.
Meneja huyo aliwaomba watanzania kuendelea
kufanya manunuzi yao katika maduka ya Mlimani City, kutokana na kuwajali wateja
wake na kutoa huduma zinazokwenda na wakati na hasa katika kipindi hiki cha
X-Mas na Mwaka Mpya.
No comments