MBUNGE WA UKONGA AFANYA ZIARA KATA YA BUYUNI KUKAGUA MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA 2016/2017 PAMOJA NA KUPOKEA KERO ZILIZOPO KWA SASA
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara (wapili
kulia) akikagua karavati ambazo zitawekwa katika kivuko cha mto Mzumbwi uliopo katika kata ya Buyuni mtaa
wa Mgeule juu katika ziara ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara (wapili
kulia) akiwa katika Mtaa wa Nyeburu katika ziara ya ukaguzi wa miradi
iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero za wananchi jijini
Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mgeule,John Matebelwa (katikati)
akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara maendeleo ya ujenzi wa
ofisi ya serikali ya mtaa huo baada ya kuwasili kwaajili ya ziara ya ukaguzi wa
miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero za wananchi jijini
Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara (kushoto) akiangalia
daraja la miti la Kidongo chekundu lililopo katika mtaa wa Zavala ambalo ni
kero kwa wakazi pindi maji yanapojaa huwa ni shida kwa zoezi la kivuko.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara(katikati)
akiwasikiliza wakazi wa mtaa wa Zavala jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwasili kwaajili ya ziara ya ukaguzi
wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akikagua ujenzi wa vyoo vya Shule
mpya ya msingi ambavyo vipo kwenye hatua ya kuezeka mabati.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akikagua ujenzi wa shule mpya ya msingi iliyopo katika mtaa wa Zavala ambayo
ina madarasa manne (4) tayari yamekamilika na mawili yanayojengwa kwa nguvu za wananchi
yameshafungwa msingi pamoja na kujazwa kifusi katika ziara
ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero
za wananchi jijini Dra es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akizungumza
na wajumbe wa Kamati ya umeme wa mtaa wa Zavala ubalozi no.7 katika ziara yake
ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero
za wananchi jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara (kulia)
akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi za Serikali ya Mtaa
wa Tallian katika ziara ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa huo,Abdallah Ungamange.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara (Kushoto)
akimueleza jambo Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Tallian,Abdallah Ungamange
(wapili kulia) baada ya kutembelea katika mtaa huo kwa ajili ya ziara ya ukaguzi
wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikiliza kero za wananchi
jijini Dar es Salaam jana.Wapili kushoto ni Katibu wa CDM kata ya Buyunu,Kamanda
Mwinuka.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akikagua moja
ya karavati zilizowekwa katika mtaa wa Tallian kwa ajili ya ujenzi wa vivuko.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akiangalia
eneo mojawapo linalohitaji kivuko katika mtaa wa Tallian kwa ajili ya vivuko
baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akiwa katika
kijiwe cha wacheza bao katika mtaa wa Kigezi pamoja na kuwasikiliza kero zao
baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara akisaini
kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi Kigezi.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mhe.Mwita Waitara (kushoto)
akikagua madarasa ya Shule ya Msingi Kigezi yaliyojengwa na Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi
iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pamoja na kusikliza kero za wananchi jijini
Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la
Ukonga Mhe. Mwita Waitara jana amefanya ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa
na Halmashauri ya Ilala pamoja na kupokea kero zilizopo kwenye mitaa sita (6)
kati ya mitaa nane (8) ya Kata ya Buyuni
Mitaa aliyofika Mhe.
Mbunge jana ni Zavala,Mgeule,Mgeule juu,Tallian,Kigezi na Nyeburu
Mtaa wa Zavala
mradi uliotekelezwa na Halmashauri ya Ilala kupitia ufuatiliaji wa Mhe. Mbunge
ni ujenzi wa shule mpya ya msingi ambayo madarasa manne (4) tayari yamekamilika
na mawili yanayojengwa kwa nguvu za wananchi yameshafungwa msingi pamoja na
kujazwa kufusi na umaliziaji wa jengo la vyoo vya wanafunzi upo mbioni
kukamilika kwani wapo kwenye hatua ya kuezeka mabati.
Changamoto zilizopo
mtaa wa Zavala ni mahitaji ya ujenzi wa vivuko eneo la Nyamalonda, Kidongo
Chekundu pamoja na mradi wa umeme kufika Kidongo Chekundu balozi No' 7 ambapo
wananchi hawakufikiwa na mradi huo kwa awamu ya kwanza Tanesco walipofanya
Survey
Mgeule changamoto
zilizopo ni umaliziaji wa jengo la ofisi ya Serikali ya mtaa pamoja na
ujenzi wa Vivuko viwili ambayo ni Mzumbwi one na Mzumbwi two
Mgeule juu
changamoto zilizopo ni uwekaji wa Karavati kwenye mto Mzumbwi ambazo tayari
zimeshafika eneo zinapohitajika kuwekwa
Tallian kuna uhitaji
wa ujenzi wa ofisi ya Serikali ya mtaa ambapo uwanja tayari
umeshapatikana kutoka kwa mwananchi aliejitolea bure pamoja na ujenzi wa vivuko
viwili ambavyo Karavati zake nazo zipo eneo tayari
Kigezi mradi
uliotekelezwa na Halmashauri kupitia ufuatiliaji wa Mhe. Waitara ni madarasa
mawili (2) ya shule ya msingi Kigezi na changamoto iliopo ni uhitaji wa
madarasa zaidi kwani jengo la zamani limepata ufa ambao haurekebishiki kwa
jinsi jengo lilivyochakaa sehemu kubwa.
Nyeburu
panahitaji matengenezo ya barabara ya mtaa eneo la Shule ya Sekondari Nyeburu.
Kupitia ziara hiyo ya
Mhe. Waitara amewashukuru wanananchi kwa jinsi wanavyompa ushirikiano katika
majukumu yake Jimboni na amewaahidi kushughulikia changamoto zote kwa
kushirikisha mamlaka za serikali zinazohusika.
No comments