WAITARA AITIKA WITO WA WAKAZI WA PUGU
Mbunge wa Jimbo la
Ukonga Mh.Mwita Waitara (kushoto) akizungumza na wakazi Kata ya Pugu Mtaa wa
Bombani jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa wakazi hao kujadili masuala
ya upimaji ardhi pamoja kusikiliza kero nyingine za Kata kwa ujumla.Katika
mkutano huo Mbunge alikuwa ni Mgeni rasmi.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Pugu Mtaa wa Bombani wakisikiliza kwa makini mada zitolewazo
na Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara pamoja na
viongozi wengine katika mkutano wa wakazi hao kujadili masuala ya upimaji ardhi
jijini Dar es Salaam.
Na mwandishi wetu
Mbunge wa Jimbo la
Ukonga Mhe.Mwita Waitara ameshiriki Mkutano wa wananchi wa Kata ya Pugu mtaa wa
Bombani jijini Dar es Salaam jana baada ya kualikwa na Diwani wa Pugu,
Bonventure Mphuru
Agenda kuu ya Mkutano
huo ilikuwa ni upimaji ardhi zoezi ambalo liliibuliwa na wananchi na baadae
wakawasillisha kwa viongozi wa mtaa wao na Kata
Mengineyo yaliyojitokeza
kwenye mkutano huo ni masuala ya barabara mbovu eneo la Kisumu kuelekea kwa IGP
mstaafu Mzee Mwema kwani mvua zikinyesha kidogo njia hiyo haipitiki
kabisa .
Mhe. Mbunge amewaahidi
atawasiliana na diwani ili wapate ufumbuzi wa barabara hiyo kwa kuwasumbua
Wakala wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA)
Pia Mhe. Mbunge
amewasihi wananchi waiamini kamati ambayo inasimamia zoezi la upimaji ardhi ili
wafikie malengo waliojiwekea wenyewe kwani kamati ni miongoni mwa wananchi
walioomba kupimiwa maeneo yao
Mwisho Mhe. Mbunge
amewaomba wananchi wa Pugu watumie nafasi ya upendeleo kufika ofisi ya Mbunge
kila Jumatano kuonana nae yeye mwenyewe kwani ofisi ipo kwenye Kata yao hakuna
gharama kumuona Mbunge.
No comments