Airtel yatangaza kuongeza GB bando za Yatosha Intaneti,
Meneja Masoko Airtel
Tanzania Aneth Muga, akitoa Maelezo wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali
nchini kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti
zinazotolewa na Airtel kupitia bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha
Intaneti’ .
Baadhi ya watangazaji wa
radio mbalimbali nchini wakifuatilia mada kwa umakini wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali nchini na Airtel
kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na
Airtel kupitia bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel Tanzania imekutana na watangazi wa radio mbalimbali
nchini na kuongelea ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti
zinazotolewa na Airtel kupitia kuzinduliwa kwa bando mpya za ‘SMATIKA na
Yatosha Intaneti’ zilizozinduliwa mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo lengo
la kuwapatia wateja na watumiaji wote wa intaneti bando nafuu zaidi.
Meneja Masoko Airtel
Tanzania Anethy Muga alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’
zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote,
na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha
Intaneti kwa kujipatia bado za gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kupata MB
40. Vilevile ofa kabambe ya ‘SMATIKA Yatosha bando’ itamuwezesha mteja wa
AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo
kwa shilingi elfu mbili tu”
kwa upande wake Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Yatosha mpya inakupa bado za siku,
wik, mwezi gharama nafuu kuliko zote nchini, kwa mfano bado ya 5,000 zamani ilikuwa
na GB 1, kwa sasa Yatosha Intaneti Mpya unapata GB 2 kwa siku 7,
vile vile kwa shilingi 10,000 zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7
lakini sasa tumeliongeza zaidi unapata GB 6 zakutumia wiki nzima. Alieleza Muga
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’
ni ishara ya Airtel kuanza vyema shamrashamra kusherehekea sikukuu kwa
kuwapatia uhakika wateja na watumiaji wa huduma ya intaneti wa kutoishiwa bando
kwa muda mfupi,
Ukiwa na Airtel Yatosha Intaneti hainaga
kuzima data tena!” Alisisitiza Mmbando.
No comments