Breaking News

WAAJIRI WASHAURIWA KUPELEKA MICHANGO KWA WAKATI NSSF

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Samwel Wangwe (kushoto), akikabidhi tuzo kwa Ofisa Malipo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Fredrick Mbise baada ya kampunio hiyo kuibuka washindi kati ya makampuni ya uzalishaji yaliyolipa michango ya wafanyakazi wao kwa wakati katika Mfuko wa NSSF. Hafla hiyo ilifanyika mjini Arusha hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi za Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Godius Kahyarara.

NA MWANDISHI WETU

WAAJIRI nchini wameshauriwa kufikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kuwawezesha  wafanyakazi wao kunufaika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.

Ushauri huo umetolewa na Meneja  Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Bi. Diana Malambugi wakati wa mahojiano maalumu yalifanyika mjini Tanga jana alipokuwa akizungumzia tuzo waliyopewa ya Muwasilisha Michango kwa Wakati katika Sekta ya Viwanda na Mfuko wa Taifa wa  Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati wa mkutano wake mkuu mjini Arusha.

Meneja huyo alisema baadhi ya waajiri wanashindwa kupeleka kufikisha michango ya waajiwa wao kwa wakati au kutoipeleka kabisa kuwasababishia usumbufu mkubwa pindi wanapofika katika ofisi za mfuko huo kudai stahili zao.

“Kuna mafao mengi ya NSSF kwa wanachama wake mfano, mafao ya matibabu, uzazi na pensheni za uzeeni, urithi, ulemavu na mengineyo, mwanachama ambaye michango yake haifikishwi NSSF hawezi kunufaika na mafao haya,” alisema.

Akizungumzia siri ya kushinda tuzi hiyo, Bi. Diana alisema ni kutoka na na utaratibu mzuri kuanzia michango hiyo inavyokatwa kiutoka katika mishahara ya wafanyakazi mpaka inapowasilishwa katika mfuko huo.

“Ushindi wetu unaleta faraja kwa wafanyakazi wetu kuwa michango yao inafikishwa mahali panapotakiwa hivyo kuongeza imani na ari ya uzalishaji mali kwa wafanyakazi wetu,” aliangeza meneja rasilimali huyo.

Akizitaja baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia baadhi ya waajiri kushindwa kabisa au kuchelewa kufikisha michango NSSF kwa wakati meneja huyo alibainisha kuwa ni baadhi ya waajiri kutokuwa na mfumo mzuri (mechanism) katika suala zima la uandaaji mishahara na uwasilishaji makato.

Aidha alitaja sababu nyingine kuwa ni utashi wa baadhi ya  waajiri katika kuhakikisha wanalipa asilimia 10 ya mshahara wa wafanyakazi wao ili kuongezea asilimia 10 ya mfanyakazi jambo ambalo pia kwa baadhi linachangiwa na biashara kutokwenda vizuri.

Kampuni ya Saruji Tanga inayofanya biashara yake kwa kutumia chapa ya Simba imeandikishwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ina wanachama 124  katika mfuko wa NSSF.

No comments