Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,
Mwajuma Majid Abdalla (kushoto) mabati yaliyochangwa na wadau mbalimbali
aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi
ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya
mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya
Meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, nondo zilizochangwa na wadau
mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba
za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba.
Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo
yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla.
Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa
Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba, Omari Khamis Othman, mifuko ya saruji iliyochangwa na wadau mbalimbali
aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi
ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya
mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya
meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani mara baada ya meli hiyo kuwasili
na mizigo hiyo kutoka jijini Dar es Salaam.
NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewahamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo
nchini na kufanikisha kupata vifaa vya ujenzi wa mradi wa awamu ya kwanza wa
nyumba za Polisi Mikoa ya Pemba, Zanzibar.
Mradi huo umeanza katika Mikoa ya Kusini Pemba
na Kaskazini Pemba ambapo nyumba kumi na mbili zinatarajiwa kujengwa ili
kufanikisha askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi ndani ya mikoa hiyo waweze
kuishi katika nyumba za jeshi pamoja na kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa
nyumba za makazi ya polisi hao, pia mradi huo utajenga nyumba katika mikoa
mipya nchini pamoja na makao ya nchi Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa
hivyo, katika Bandari ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba, jana, Mhandisi
Masauni alisema, ujenzi wa nyumba hizo utakua ni wa hatua ya awali, lakini
mipango mbalimbali itaendelea kuwezesha nyumba nyingi zaidi kujengwa katika
eneo hilo ili kuhakikisha baadhi ya askari wanaoishi nje ya kambi za polisi
waweze kuishi kambini ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendelea kufanya kazi
kwa ufanisi mkubwa zaidi.
“Leo nimewakabidhi wakuu wa mikoa hawa vifaa
vya ujenzi ambavyo ni mifuko ya saruji, nondo, ndoo za rangi na mabati ili
waweze kusimamia zoezi hili la ujenzi wa nyumba za askari wetu kwa umakini
mkubwa,” alisema Masauni na kuongeza;
“Tunajenga nyumba hapa Pemba ni mradi wa awamu
ya kwanza, kwa awamu ya pili tutaenda katika maeneo mengine ya nchi, hususani
mikoa mipya yaSimiyu, Geita, Katavi na Songwe na pamoja na Makao ya nchi
Dodoma, kwa kuwa askari wetu hawa wanafanya kazi kubwa sana kwa kuwalinda raia
wa nchi hii kuendelea kuwa salama kwa wao wenyewe pamoja na mali zao.”
Alisema anawashukuru wadau mbalimbali kwa
kujitolea kutoa vifaa hivyo ili kufanikisha suala hilo na aliwataka watanzania
wawe na moyo kama wadau hao kwa kuipenda nchi yao, kupenda maendeleo kwa kutoa
misaada mbalimbali.
Masauni alifafanua kuwa, suala la maendeleo
halina siasa, tuijenga nchi, katika mazingira mengi ya Tanzania Bara na
Zanzibar kwa maana ya Unguja katika suala la kujitolea wamekua wanafanya hivyo,
ila kuna changamoto kidogo kwa upande waPemba pana tatizo la masuala ya
kisiasa, watu wamekua wakiingiza siasa mbele katika masuala ya nchi katika
mikoa hiyo ya Pemba, ambapo alisema jambo hilo sio jema katika maeneleo ya
nchi.
“Serikali zote mbili ya Bara na Visiwani zipo
kuwahudumia wananchi wote, wakati wa siasa umepita, sasa hivi tunataka kila
mmoja ashiriki katika masuala yote ya kimaendeleo, askari hawa wanaangalia
usalama wa watu wote, bila kujali hitikadi, dini ya mtu, wapi anatoka, bila
kujali rangi yake bila kujali kabila lake,” alisema Masauni.
Alisema viongozi wa Serikali katika mikoa ya
pemba wamekua wakipata tabu kuhamasisha katika masuala mbalimbali ya maendeleo
katika maeneo yao, hivyo wao kama serikali kuu wameamua kupeleka maendeleo
katika maeneo ambayo yanakua yana tabu katika kuhamasisha masuala ya maendeleo,
hivyo wakaamua waje mikoa hiyo ya Pemba katika awamu hiyo ya kwanza ya mradi.
Akizungumzia ujio huo wa Naibu Waziri pamoja
na ujenzi wa nyumba hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla,
alisema anamshukuru kiongozi huyo kwa kuwaletea maendeleo hayo makubwa ya
ujenzi wa nyumba za polisina kumuhkikishia vifaa walivyopokea watasimamia
ujenzi wa nyumba hizo kwa nguvu zao zote.
“Sisi wakuu wa mikoa tunakushuru naibu waziri
kwa hili ulilolifanya, tunakuhakikishia tutasimamia ujenzi huu kwa juhudi zote
mpaka nyumba zitakapokamilika, tunasema asante sana kwa kuhamasisha wadau na
hatimaye kufanikiwa kupata vifaa hivi,” alisema Mwajuma.
No comments