Breaking News

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameliagiza jeshi la Polisi nchini, kuendelea kuwapa kipaumbele askari wa kike katika mafunzo mbalimbali ili waweze kukabiliana na vitendo vya uhalifu mpya ambao umeanza kushika hatamu ukiwemo ugaidi, uchochezi, uhafidhina, wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao, utakatishaji wa fedha haramu, ujangili, usafirishaji wa dawa za kulevya na makosa mengine yanayovuka mipaka.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo  jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifunga maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania(TPF NET) katika viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini yaliyokuwa na kauli mbiu ‘Usalama Wetu ni Mtaji wa Maendeleo, Tokomeza Uhalifu Kuwezesha Uchumi wa Viwanda”.

“Tumeona juhudi zenu kwa kudhibiti uhalifu katika maeneo yaliyokuwa korofi, ila ni jukumu lenu pia kuhakikisha kuwa mnakabiliana na vitendo hivyo vya uhalifu,kuhakikisha havivurugi hali ya amani na kuhatarisha usalama wa nchi”amesema .

Ameweka wazi kuwa ni wazi kwamba shughuli za kiuchumi zitafanyika kikamilifu iwapo nchi itakuwa tulivu na yenye amani na kwamba amani na utulivu huo,ndiyo utaleta kuaminiana na kukubaliana miongoni mwa wananchi na wawekezaji, hivyo suala la ulinzi na usalama ni muhimu katika maendeleo na ustawi wa nchi.

Alisema pamoja na kwamba jeshi hilo limejenga madawati ya jinsia ili kukabiliana na tatizo hilo lakini kuna umuhimu wa kuzidisha utoaji wa elimu kwa jamii ili kuwaelewesha kuwa wasiwe waoga wala wasione aibu kuripoti matukio hayo.


Hata hivyo alisema, Serikali inajitahidi kuboresha jeshi la polisi kwa kuendelea kulipatia vitendea kazi na itazidi kufanya hivyo kulingana na bajeti iliyopo sambamba na kushirikiana na wadau wenye nia njema ya kuwasaidiia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la polisi wanawake kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya umuhimu wa alama za barabarani kutoka kwa Koplo Faustina Nduguru wa Kitengo cha Usalama Barabarani makamo makuu ya polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu kamera kugundua wanaoendesha kwa mwendo mkali kutoka kwa Konstabo Sharifa Ismail wa Kitengo cha Usalama Barabarani makamo makuu ya polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments