Breaking News

RC MAKONDA AZIDI KULETA NEEMA KWA WAKAZI WA DSM.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wa pili (kushoto) akishikana mikono na meja wa jeshi la china Xing song.



Makonda akizungumza na waandishi wa habari pamoja wa wadau wa sekta ya afya kutoka China na Tanzania.


 Madaktari bingwa na wataalamu wa afya 381 kutoka Jeshi la China wanatarajiwa kuwasili kwa meli katika bandari ya Dar es salaam tarehe 19 Novemba 2017 kwa ajili ya kufanya matibabu bure kwa wakazi wa Jiji la DSM kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA katika kuwahudumia wananchi. 


Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA amesema madaktari hao watahudumia wananchi 600 kwa siku ndani ya meli hiyo ambapo matibabu ya kawaida pamoja na upasuaji utafanyika bure ndani ya meli hiyo na kuwataka wakazi wa DSM na  wananchi wote kwa ujumla kutumia vyema fursa hiyo itakayodumu kwa siku 7. Jijini hapa pia amesema watanzania  wataendelea kupata neema  kama wataendeeleea kumchagua na kumuamini Rais wetu John Pombe Magufuli katika utawala wake.

No comments