YAS WASHINDA TUZO TATU ZA TEHAMA 2025
Kampuni ya Mawasiliano ya YAS imekua ya kwanza nchini kushinda Tuzo Tatu za TEHAMA 2025 , Tuzo zilizoandaliwa na Tume ya TEHAMA ( ICTC ) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambapo Mgeni rasmi alikua Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Slaa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt. Nkundwe Mwasaga, na kupokelewa na Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji na Afisa Mkuu wa Fedha - YAS Bwn. Innocent Rwetabura.
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni namba Moja nchini kwa Utoaji wa huduma za Kidigitali YAS imeibuka mshindi wa Tuzo Tatu za TEHAMA katika Vipengele vifuatavyo Best use of ICT & Social Impact _ Mtumiaji Bora wa TEHAMA & Manufaa kwa Jamii, Best Internet Service Provider - Huduma Bora za Intaneti na Best Mobile Network Provider - Kampuni Bora ya Mawasiliano , Tuzo zilizotolewa hivi karibuni Jijini Arusha .
Lengo kuu la kutoa Tuzo hizi ni kutambua mchango mkubwa wa uwekezaji , Utoaji Huduma na Ubunifu unaofanyika katika sekta ya TEHAMA .
Ikumbukwe kampuni ya YAS imekua ikishinda TUZO mbalimbali za Kimataifa ikiwemo Tuzo ya Mtandao wenye Intaneti yenye Kasi zaidi kutoka Ookla , YAS wameshinda Tuzo hii mara mbili mfululizo.
Post Comment
No comments