Breaking News

WATANZANIA WAIBUKA KIDEDEA YAS KILI HALF MARATHON 2025

Kilimanjaro, 23 Februari 2025: Katika mbio za YAS Kili Half International Marathon Km 21 zilizofanyika mkoani Kilimanjaro mapema leo , Mtanzania, Inyasi Sule ( Pichani ) ndiye ameibuka mshindi kwa kumaliza mbio hizo kwa saa moja dakika 3 na sekunde tano, Inyasi amefuatiwa na Watanzania wenzake Samhenda Sombi , Peter Mwangi , Joseph Panga , Yohani Elisante , Shumeli Said , Gervas Mayo , na Yohana Sulle huku nafasi ya 6 ikichukuliwa na Raia wa Kenya Benard Kiplagat na Nafasi ya 8 imekukuliwa na Raia wa Rwanda Theophile Rugamba.

Mbio za Kili International Marathon zinazoshirikisha wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni ambapo kipengele cha km 21 maarufu kama Half Marathon kinadhaminiwa na Kampuni ya mtandao wa simu ya Yas kwa mwaka wa kumi sasa na mwaka huu 2025 washiriki zaidi ya 2000 wameshiriki mbio za Yas Marathon.

Picha za matukio mbalimbali jinsi wafanyakazi wa YAS walivyozinogesha mbio hizo















.

No comments