Breaking News

YAS WAPONGEZWA KWA KUJALI UTUNZAJI WA MAZINGIRA KARIBU NA MLIMA KILIMANJARO


Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe.  Godfrey Mnzava akirudishia udongo kwenye mti,baada ya kuotesha jana katika kijiji cha sango kata ya Kimochi,ikiwa ni sehemu ya utunzaji wa mazingira katika Mkoa wa Kilimanjaro, miche ya miti hiyo ilitolewa na kampuni ya mawasiliano ya YAS,inayo dhamini mbio za kimataifa za Kili Marathon kilomita 21

Mkuu wa Wilaya  ya Moshi Godfrey Mnzava akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Kijiji cha Sango kata ya Kimochi, kupitia kampeni ya Kampuni ya mawasiliano ya Yas ,zoezi hili lilifanyika kijijini hapo wakishirikiana na wafanya kazi wa kampuni ya mawasialano ya YAS.

Wananchi wa kijiji cha sango kata ya kimochi Wilaya ya Moshi,wakishiriki zoezi la kuotesha miti kwenye eneo la kijiji hicho, miche hiyo ya miti ilitolewa na kampuni ya mawasiliano ya YAS ,inayodhamini mbizo za kilomita 21 maarufu kama Yas Kili - Half Marathon ambapo kwa mwaka huu wa 2025 ni kwa mara 10 sasa kampuni ya Yas imekua ikidhamini mbio hizo.

Na Mwandishi Wetu - Moshi

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imeipongeza kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania kwa kazi kubwa ambayo inafanya kwa kupanda miti pamoja na shughuli zingine zinahusiana na uhifadhi wa mazingira, pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu wakati wa hafla ya kampeni ya kupanda miti iliyofanyika kata ya Kimochi, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa wiki hii.

Katika risala iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Moshi Bw Gidfrey Mnzava, Bw Babu alisema kuwa kamepni ya upandaji miti iliyofanywa na kampuni hiyo haina budi kuwa endelevu ili kuendelea kulinda mazingira na uhifadhi wake kwa ujumla.

“Niwapongeze Yas na wadau wengine walioshirikiana nao kwa kazi nzuri hii haswa ikitiliwa maanani ya kuwa changamoto kubwa inayoikabili dunia ni mabadiliko ya tabia nchi ambayo njia pekee ya kukabiliana nayo ni upandaji wa miti kwa wingi na kuhifadhi mazingira”, alisema.

Aliongeza, “Tunahitaji kuwa na mazingira mazuri maana tunayategemea kwa shughuli zetu za kila siku ikiwemo upatikanaji wa raslimali nyingi ambazo tunahitaji kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali muhimu kwa binadamu; hatuwezi kukwepa wajibu wa kuyatunza mazingira kutokana naumuhimu wake huo”.

Alisema kuwa ni jukumu la kila taasisi na mtu mmoja mmoja kuhakikisha kuwa miti inapandwa kwa wingi wakati huo huo kuhakikisha kuwa inatunzwa na kukua kutokana na ukweli kuwa mazingira yakiharibika na maisha ya wanadamu yatakuwa magumu.

“Nichukue fursa hii kuendelea kuwasihi viongozi wetu wa Kidini kuendelea kuungana na Serikali katika kuwahamasisha watu kuendelea kupanda miti na pia kuhakikisha wanayatunza mazingira ili Taifa liendelee kuwa mahali salama pa kuishi”, alisema.

Akikongea katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Yas Bw Innocent Rwetabura, alisema kampuni hiyo imelenga kupanda zaidi ya miti 25,000 kwa mwaka wa 2025, kupitia kampeni iliyobeba kaulimbiu Green for Kili, Hatua Moja Mti Mmoja.

Alisema kampeni hiyo imelenga kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira na uhifadhi wa amazingira kwa ujmla ikiwemo kuhakikisha kila halmashauri inapanda miti milioni 1.5 kwa mwaka.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wadau wengine ambao wanaungana na sisi katika kampeni hii, ambao nia pamoja na WWF, Pangani Basin Water Board (PBWB), hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na halmashauri ya wilaya ya Moshi (MDC)”, alisema.

Kwa upande wake mwakilishi wa WWF katika hafla hiyo Bi Joan Itanisa alisema taasisi hiyo imeendelea kuungana na wadau wengine wa mazingira katika kuhakikisha pamoja na mambo mengine uoto wa asili unarudi.

“Takwimu zinazotolewa na wataalam mbalimbali wa mabadiliko ya tabia nchi na mazingira zinaonyesha ni namna gani hali ya ikolojia ya Mlima Kilimanjaro inavyozidi kudhoofu; ndiyo maana WWF tumekwua tukifanya kazi kwa muda sasa kunusuru ikolojia hii muhimu kabisa kwa nchi yetu na Afrika kwa ujumla”, alisema.

Naye mwakilishi wa KINAPA Bw Mdesa Mapinduzi aliipongeza kampuni ya  Yas kwa juhudi inazofanya kuhakikisha mazingira haswa yanayozunguka Mlima Kilimanjaro yanaendelea kuwa mazuri.

“Katika ushirikiano huo, umetuwezesha KINAPA kupanda miti zaidi ya 30,000 na pia kuanzisha vitalu vya miche ya miti; tayari tuna zaidi ya miche 200,000 kwenye vitalu hivyo”, alisema.

Mwakilishi kutoka PBWB Bi Arafa Majid, alisema kuwa taasisi hiyo inasimamia jumla ya vyanzo vya maji 762 vilivyoko mkoani Kilimanjaro na ambavyo alisema kuwa vyote vinahitaji kuhifdhiwa ili kupatikane maji ya uhakika kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya binadamu.

“Chanzo hiki kilichoko hapa Kimochi ni moja wapo ya vyanzo hivyo na leo hii tutapanda miti 200 kwa ajili ya kukihifadhi; hii ni hatua nzuri ambayo hatuna budi kuwashukuru Yaa Tanzania kwa kuja na kampeni hii”, alisema.

Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Moshi (MDC) Bw Shadrack Mhagama, alitoa rai kwa wananchi kuacha kukata miti kiholela na kwamba kama kuna ulazima wa kufanya hivyo wahusika hawana budi kufuata taratibu zilizoko kabla ya kukata miti.

"Hata kama mti umepuanda wewe, ni lazima upate kibali kutoka Seriakalini ambacho hutolewa na Mkuu wa Wilaya tu; fuata taratibu zilizoko na kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo utapata kibali kutoka kwa mamlaka husika kukata mti huo", alisema.

No comments