Breaking News

DAR ES SALAAM MWAMKO NI MKUBWA KUELEKEA YAS KILI HALF MARATHON 2025

Na Mwandishi Wetu.

Februari, 14 - 16,  2025 Maelfu ya wakazi wa Dar Es Salaam , wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Mlimani City kwa ajili ya kuchukua Namba na Vesti ya kukimbilia kuelekea mbio kubwa za kimataifa maarufu kama Yas Kili Half International Marathon , Mbio hizi ambazo zinatarajiwa kufanyika Februari 23, 2025 , ambapo hadi sasa Yas wamekua wakidhamini mbio hizi ( HALF MARATHON 21 KM ) kwa miaka  10 mfululizo. Mbio hizi maarufu  huwakutanisha washiriki zaidi ya 12,000 kutoka nchi takribani 55, na kupelekea kukuza vipaji na uchumi wa Taifa. 

                              

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti baadhi ya Washiriki wa Yas Kili Half International Marathon 2025 wameonyesha mwamko wa hali ya juu na shauku yao kubwa ya kushiriki mbio hizi za kimataifa . 

Kwa upande wake Sammfredrick Coleman Mkimbiaji Wa Yas Kili Half International Marathon 21 KM ambaye pia ni mkimbiaji wa mbio hizo kwa muda sasa amesema amejipanga kwa hali ya juu kushiriki mbio hizi 

" Asante sana Yas kwa Udhamini wa Half Marathon , hakika tumejionea tangia jana na leo mwamko ni mzuri watu wengi wamejitokeza hapa katika viwanja vya Mlimani City kwa siku ya jana na leo kwa ajili ya kujisajili , lakini ambao hamjajisajili hapa ratiba bado inaendelea Kwa Arusha na Moshi , Asanteni na tupo tayari kwa Yas Kili Half International Marathon 2025 ". 

Naye kwa upande mwingine Mkimbiaji wa 21 KM Bwn. Haji Katembo kutoka Kigamboni Jogging amewapongeza Yas kwa udhamini wao kwa miaka kadhaa mfululizo na kusisitiza kuwa yupo tayari kwa mbio Februari 23.

Ikumbukwe , Ratiba ya Vituo vya kuchukua namba na Vesti za kukimbilia baada ya Dar Es Salaam itaendelea Arusha na Moshi.

















No comments