YAS WAMPA MILIONI 10 MTEJA WAO KUTOKA MOROGORO
Kampuni ya mawasiliano ya Yas kupitia ofisi yake iliyopo manispaa ya Morogoro, imemzawadia Sadam Hamisi mkazi wa Manispaa hiyo hundi ya shilingi milioni 10 ,(10,000,000) alizojishindia kupitia droo ya 11 ya promosheni ya Magift ya Kugift, inayochezeshwa na kampuni hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi hiyo, Sadam ameeleza kuwa amefanikiwa kushinda kutokana na juhudi zake za kufanya miamala mbalimbali kupitia huduma ya Mixx by Yas Miamala hiyo ilihusisha kuweka na kutoa fedha, kununua vifurushi vya dakika, SMS, na intaneti, pamoja na kulipia bidhaa kwa njia ya Lipa Namba.
Aidha Sadam ameongeza kuwa fedha hizo atatumia kuongezea mtaji wa biashara ya viatu aliyokuwa akifanya pamoja na kufungua ofisi ya biashara ya vifaa vya umeme na ufundi na fedha zingine atatumia kuwasaidia wazazi wake, ambapo pia alatumia wasaa huo kuwahimiza watumiaji wa simu za mkononi kuendelea kuamini huduma za Yas na kuongeza matumizi ya huduma za Mixx by Yas kwa kufanya miamala mara kwa mara.
Kwa upande wa meneja wa Yas, Manispaa ya Morogoro, Gwamaka Mwakilembe amesema kuwa kampeni ya Magift ya Kugift ilianza mwaka jana 2024 ikiwa na lengo la kurudisha kwa wateja kwa kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kuweka na kutoa pesa ambapo wateja waliweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku,wiki na mwezi.
Mwakilembe ameongeza kwa kusema kuwa kampeni ya Magift ya Kugift imefikia kikomo na kua kuisha kwa kampeni hiyo ni mwanzo wa kamoeni nyingine nyingi za kuwafikia wateja.
Promosheni ya Magift ya Kugift ilikua na lengo la kuwanufaisha wateja wa Yas na mawakala wake kwa kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu kuanzia shilingi laki moja hadi milioni kumi, simu janja (smartphones), na gari jipya lenye kilomita sifuri (0 km).
No comments