MSHINDI MWINGINE WA MILIONI 50 KUTOKA YAS ATOKEA RUVUMA
Mkazi wa Songea Mkoani Ruvuma Bw. Christian Ndunguru ( wa pili kulia ) ameshinda kupitia promosheni ya Magift ya kugfti Shilingi Milioni 50 kwa kutokana na kufanya miamala kupitia MIXX BY YAS ( Zamani Tigo Pesa ) , amekabidhiwa Mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 na Meneja Biashara Kanda ya Nyanda za juu Kusini Ronal Richard ( Kushoto ).
Na Mwandishi Wetu.
Ruvuma, 13 Februari 2025: Kampuni ya mawasiliano ya Yas kupitia ofisi yake iliyopo Manispaa ya Songea, imemzawadia Christian Nduguru mkulima na mfanyabiashara Songea mkoa wa Ruvuma kiasi cha Tsh Milioni 50 kama mshindi wa Kampeni ya Magift ya Kugift’ droo ya 12 na ya mwisho.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi hiyo, Meneja Biashara Yas, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ronald Richard ameeleza kuwa wao kama kampuni wamefanikiwa kukamilisha kampeni hiyo na hatimaye, Bwana Nduguru ameibuka mshindi wa mil 50, ambapo anatoka kwenye kanda yake.
Kampuni ya Yas kupitia kitengo cha Mixx by Yas imekuwa ikiendesha kampeni hiyo ambayo ilianza mwishoni mwa mwaka jana ambapo hadi kufikia leo Februari 13 zaidi ya washindi 300 wameweza kujishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo simu na pesa taslimu.
Kwa upande wake mshindi wa zawadi hiyo, Bw Ndunguru, “amesishukuru kampuni ya Yas kwa kuendesha kampeni hiyo na kusema zawadi hiyo ni ya Wanasongea wote kwani fedha hizo atazitumia ndani ya mkoa huo”.
Aidha Ndunguru amesisitiza kuwa yeye kama mteja mwingine amekuwa akishiriki mara nyingi kucheza ikiwa ni pamoja na kutuma miamala, kununua vitu mbalimbali kupitia Mixx by Yas na hatimaye sasa bahati imeangukia kwake amesema, Ndunguru.
Kampuni ya Yas Tanzania kupitia kitengo cha Mixx by Yas imekuwa ikirudisha hisani kwa jamiii kwa kuchezesha kampeni mbalimbali Nchini ilikuwa karibu na Wananchi.
No comments