Breaking News

TBS WAFANYA KIKAO NA WADAU WA MIFUKO MBADALA NA VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI

 

Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Dkt.Athuman Ngenya akiongoza Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Viwango (TBS), Bw. David Ndibalema, Mkurugenzi wa Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi Redempta Samwel na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Dkt.Candida Shirima pamoja na Kaimu Meneja wa Ukaguzi na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Bw.Moses Mbambe Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Dkt.Athuman Ngenya akifungua Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. 


Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Dkt.Candida Shirima akizungumza katika Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam.   Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki wakiwa katika kikao ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kikao hicho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki wakiwa katika kikao ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kikao hicho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam.

(PICHA -  EMMANUEL MBATILO)

*********************


Mifuko mbadala na vifungashio vya plastiki hutumika kwa namna mbalimbali, hivyo endapo hazitadhibitiwa kikamilifu huweza kusababisha athari katika mazingira na vilevile, endapo mtumiaji atanunua bidhaa zisizokidhi vigezo vya ubora kuendana na matarajio yake husababisha malalamiko.


Kwa mantiki hiyo, kila mmoja anao wajibu wa kuzingatia matwaka yote ya ubora ili kukuza pato la taifa, kupunguza gharama za udhibiti, kuleta ushindani wa haki katika biashara, kulinda mazingira, kuwezesha wanunuzi kupata bidhaa zinazoendana na thamani ya fedha wanazolipa na kuepusha malalamiko.

Ameyasema hayo leo Machi 2,2023 Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya wakati akifungua Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam.

Amesema Shirika limeandaa mkutano huo mahususi kwa lengo la kukuza uelewa wa wadau wa mifuko mbadala na vifungashio vya plastiki vilivyoruhusiwa ili waweze kukidhi matakwa ya Sheria ya Viwango Sura 130 pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Aidha Dkt.Ngenya amesema TBS inawajibika kikamilitu kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na zile zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na mifuko mbadala na vifungashio vya plastiki vilivyoruhusiwa zinakidhi matakwa ya viwango ili kukuza uchumi wa nchi yetu.

"Kwa mantiki hii, TBS itaendelea kutilia mkazo suala la usimamizi wa viwango na kudhibiti bora wa bidhaa hizo ili kuhakikisha zinakidhi vigezo vya ubora unaotakiwa". Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzingatiaji wa Sheria na Utunzaji wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi Redempta Samwel ametoa wito kwa wazalishaji na waagizaji kuzingatia viwango vilivyowekwa na TBS kuhakiisha ile dhana nzima ya ya serikali ya kuruhusu vifungashio viendelee kuwepo ili kuhifadhi ubora, haitumiki vinginevyo ili kuweza kulinda mazingira.

Pamoja na hayo amesema katika kufanya ufuatiliaji, utekelezaji na uzingatiaji wa sheria wamegundua kwamba kuna changamoto nyingi hivyo kupitia kikao ambacho TBS wamekiandaa wataenda kujadiliana kuona ni namna gani wanaweza kupunguza changamoto katika suala la mifuko mbadala pamoja na vifungashio vya plastiki.

Nae Meneja wa Masoko ya Nje wa Kampuni ya A to Z Textile Millers ambao ni Wazalishaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki Bw.Sylvester Kazi amesema kupitia kikao hicho wanakwenda kupata fursa kutoka soko dogo la Afrika Mashariki na kwenda kwenye soko kubwa zaidi ambalo ni soko huru la Afrika kwa kutambua viwango vya bidhaa na kuzalisha kwa kufuata viwango husika.

No comments