Breaking News

WATANZANIA WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA NYEMELEZI

 




Na mwandishi wetu

WITO umetolewa kwa watanzania, hususan wafanyakazi wanaotumia muda mwingi kufanya kazi wakiwa wamekaa kufanya mazoezi, ili kuimarisha afya zao na kujiepusha na magonjwa nyemelezi.

Wito huo umetolewa na Mkaguzi wa Ndani wa Benki ya Biashara ya DCB, Bwana Samwel Mahendela wakati wa mbio za mwaka huu za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon, zilizotimua vumbi katika mji wa Moshi, Mkoani Kilimanjaro Leo.

Akiongoza timu ya wafanyakazi 40 wa benki hiyo kushiriki mbio hizo mjini hapa, Bwana Mahendela alisema, mbio hizi ni muhimu hasa kwa wafanyakazi wa sekta ya mabenki kwani hutumia muda wao mwingi kuhudumia wateja wakiwa kwenye viti.

“Kushiriki mbio kama hizi pamoja na mazoezi ya viungo kwa ujumla vinaimarisha afya ya mwili na akili na kuongeza ufanisi wa kazi, mara nyingi tunafanya kazi tukiwa tumekaa na pia hatuna muda wa kutosha wa kufanya mazoezi.

“Natoa wito kwa wafanyakazi wa sekta za mabenki pamoja na watanzania kuchangamkia mbio za Kilimanjaro Marathon ili kuimarisha afya zao.

“ Natoa pongezi pia kwa benki yetu pendwa ya DCB kwa kutuwezesha sisi wafanyakazi wake kushiriki mbio hizi lakini pia kwa kuisapoti DCB runners club, DCB tupo Imara tunasonga mbele.

01
Meneja Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya Biashara ya DCB, Samwel Mahendela ( katikati) akikimbia mbio za km 21.1 na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon mjini Moshi Mkoani  Kilimanjaro. Picha nyingine ni baadhi ya wakimbiaji wa DCB wakishiriki mbio hizo.

02

03

04

05

06

No comments