MAELFU WAJITOKEZA KUCHUKUA NAMBA NA VESTI ZA KUKIMBILIA , KUELEKEA TIGO KILI HALF INTERNATIONAL MARATHON 2023.
Na Mwandishi Wetu .
Baadhi miongoni mwa Maelfu ya Wakimbiaji watakaoshiriki Tigo Kili Marathon 2023 walivyojisajili katika Viwanja vya Mlimani City , Jijini Dar Es Salaam . Vituo vinavyofuata ni ARUSHA , ambapo itakua ni Jumanne ya Tar. 21 - 22 Saa nane mchana hadi saa 12 jioni Kibo Palace Hoteli , na Moshi ni Alhamisi ya 23 hadi Jumamosi ya 25 Februari , MoCu Stadium Moshi.
Na Mwandishi Wetu.
Februari, 18 - 19 , 2023 Maelfu ya wakazi wa Dar Es Salaam , wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mlimani City kwa ajili ya kuchukua Namba na Vesti ya kukimbilia kuelekea mbio kubwa za kimataifa maarufu kama Tigo Kili Half International Marathon , Mbio hizi ambazo zinatarajiwa kufanyika Februari 26, 2023 , ambapo hadi sasa Tigo wamekua wakidhamini mbio hizi ( HALF MARATHON 21 KM ) kwa miaka 8 mfululizo. Mbio hizi maarufu huwakutanisha washiriki zaidi ya 12,000 kutoka nchi takribani 55, na kupelekea kukuza vipaji na uchumi wa Taifa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti baadhi ya Washiriki wa Tigo Kili Half International Marathon 2023 wameonyesha mwamko wa hali ya juu na shauku yao kubwa ya kushiriki mbio hizi za kimataifa . Kwa upande wake Nusrat Salum Mkimbiaji Wa Tigo Kili Half International Marathon 21 KM ambaye pia ni Msemaji wa Clouds Jogging amesema kuwa amejipanga kwa hali ya juu kushiriki mbio hizi
" Asante sana Tigo kwa Udhamini wa Half Marathon , hakika tumejionea tangia jana na leo mwamko ni mzuri watu wengi wamejitokeza hapa katika viwanja vya Mlimani City jwa siku ya jana na leo kwa ajili ya kujisajili , lakini ambao hamjajisajili hapa ratiba bado inaendelea Kwa Arusha na Moshi , Asanteni na tupo tayari kwa Tigo Kili Half International Marathon ".
Naye kwa upande mwingine Mkimbiaji wa 21 KM Bwn. Derick Mujuni amewapongeza Tigo kwa udhamini wao kwa miaka kadhaa mfululizo na kusisitiza kuwa yupo tayari kwa mbio Februari 26.Ikumbukwe , Ratiba ya Vituo vya kuchukua namba na Vesti za kukimbilia ni kama Ifuatavyo kwa Dar Es Salaam Ilikua Jumamosi ya Februari 18 - 19. Vituo vinavyofuata ni ARUSHA , ambapo itakua ni Jumanne ya Tar. 21 - 22 Saa nane mchana hadi saa 12 jioni Kibo Palace Hoteli , na Moshi ni Alhamisi ya 23 hadi Jumamosi ya 25 Februari , MoCu Stadium Moshi.
#KAZAKISHUA
No comments