Breaking News

TAASISI YA PASS TRUST IMEFANYA KONGAMANO NA WADAU WA KILIMO MKOANI KATAVI

Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya PASS Trust imefanya kongamano na wajasiliamali na wadau wote waliopo katika mnyororo wa kilimo mkoani KATAVI, ambalo linalenga kuhimiza na kutoa fursa kwa wakulima mkoani humo kupata mkopo kutoka taasisi za fedha. Ambapo wakulima wamehimizwa kufanya uzalishaji unaofuata misingi ya ukuaji wa kijani shirikishi.
Akiongea katika kongamano la wadau wa kilimo lililoandaliwa PASS, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bwana Nehemia James, amesema kuwa umuhimu wa PASS Trust unasaidia sana katika suala la kukopa huku ukisaidia Bank kuwa na uamuzi wa kutoa pesa.
Uwepo wa PASS unasaidia sana taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wakulima kutokana na dhamana zinazotolewa na PASS Trust.
Hivyo kupitia dhamana hii wakulima wanaweza kuwekeza katika kilimo ambacho kinatunza mazingira, na kinazingatia ukuaji wa kijani shirikishi, pia hii ni fursa kwa wajasiliamali wote.



No comments