Benki Ya Absa Yawataka Wanawake Kujiamini
Wito umetolewa kwa wanawake wafanyakazi pamoja na wengine nchini kujiamini wenyewe na kuwa imara ili waweze kutimiza malengo yao bila kusubiri kusukumwa kwani wanawake wamepewa uwezo mkubwa ndani yao.
Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Irene Sengati Giattas wakati wakifanya matembezi maalumu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani akihimiza wanawake mahali pa kazi kuacha woga pale wanapopata nafasi za juu za uongozi na wasisubiri kutiwa moyo bali wao wenyewe wajitie moyo na kusonga mbele.
Akitoa mfano alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ni mfano bora wa mwanamke mchapa kazi anayefanya mambo makubwa, wapo mawaziri wengi wanawake bora, wapo wabunge wengi wanawake na wapo pia viongozi wa taasisi mbalimbali wanawake wanaofanya vizuri katika utumishi wao.
Mmoja wa wafanyakazi wa Absa aliyeshiriki matembezi hayo, Aikande Kimaro alisema wameanza maadhimisho kwa kutembea kilomita nane wakisindikizwa na wafanyakazi wanaume kwa kuonyesha kuwa ushirikiano kutoka kwa wanaume ni muhimu katika kufanikisha majukumu yao mahali pa kazi na pia umuhimu wa mazoezi katika kuleta afya ya mwili na akili
Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio la matembezi hayo
No comments