TIGO WAZINDUA MNARA LONGIDO - ARUSHA
WAZIRI wa habari mawasiliano na teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye ameipongeza kampuni ya Tigo kwa kazi kubwa waliyoifanya kupunguza changamoto za mawasiliano vijijini kwa kujenga minara ambayo imekuwa chachu ya maendeleo nchini. Ameyasema hayo katika uzinduzi wa mnara wa mawasiliano ya simu katika kata ya Noondoto wilayani Longido mkoani Arusha.
" Nimezunguka maeneo mengi hasa vijijini , kuna minara mingi sana imejengwa na Kampuni ya Tigo lakini pia huduma zao ni nzuri hakika nawapongeza sana."Tutaongeza minara maeneo ambayo hasa maeneo ya mipakani nimechoka kusikia kwamba wananchi wetu wanatumia mitandao ya nchi jirani tunachotaka tuongeze nguvu ili majirani nao watumie mitandao yetu,"amesema Waziri. Aidha Waziri Nape amesisitiza wananchi kutumia huduma za mawasiliano katika chanya ili kuweza kuwasaidia katika kukuza uchumi kwani wakitumia vibaya watakutana na mkono wa sheria juu yao.
Katika azima yetu ya kuhakikisha kwamba maeneo ya vijijini yanapata muunganisho wa mtandao, Tigo imekuwa ikishiriki katika kutuma maombi ya zabuni kutoka UCSAF tangu 2012.Tunashukuru kutambua kwamba katika mengi ya matukio hayo, serikali imekuwa sikivu vya kutosha, na kutupa fursa ya kuunga mkono sera yake ya kitaifa ya ICT ambayo inaonekana kupanua mawasiliano hadi vijijini. Leo tunakabidhi mnara huu ambao tunaamini utaenda kuwahudumia watu zaidi ya 3000, vile vile tuna mpango wa kufungua maduka yatakayo hudumia wateja hawa wapya. kwa kuitimisha,naomba nichukue fursa hii kuwakaribisha wateja wetu wapya kwa huduma zetu zikiwemo Tigo pesa,usajili wa laini za simu n.k
No comments