Breaking News

WASHINDI WA DROO YA SABA Y9 MICROFINANCE WAPATIKANA

 

_L5A2403

Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Kifedha Y9 Microfinance Fredrick Mtui (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya saba kwa njia ya simu Anorld Jacob na Jekapo ambaye amejishindia simu janja wote ni wakazi wa Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa Y9 kutoa zawadi kila wiki Kwa wateja wake. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani ni Meneja Masoko ya Taasisi hiyo Bi. Sophia Mang'enya pamoja na mshindi wa pikipiki Wa droo ya sita Bw Baraka Bazarae (kushoto).

_L5A2489Meneja Masoko ya taasisi Bi Sophia Mang'enya akimkabidhi zawadi ya pikipiki mmoja kati ya washindi wa droo ya sita Baraka Bazarae katika hafla ya uchezeshwaji wa droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

_L5A2481Mshindi wa pikipiki Droo ya sita ya Y9 Microfinance Baraka Bazarae Katikati akizungumza wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance Fredrick Mtui (kulia) na Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi (kushoto).

_L5A2495Meneja Masoko ya Taasisi ya Kifedha ya Y9 Microfinance Bi Sophia Mang'enya (kulia), akimkabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya sita Baraka Bazarae ambae aliibuka kidedea wakati wakuchezesha droo ya sita wiki iliyopita makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa yakuchezesha droo kwaajili ya kutafuta washindi wa droo ya Saba. Kushoto ni Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi (kushoto).



Washindi wa Droo ya saba ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Anorld Jacob na mshindi wa simu Jekapo wote wakiwa ni wakazi wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji taasisi ya kifedha Y9 microfinance Fredrick Mtui ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.

Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mteja wa Y9 microfinance anapata nafasi ya kushiriki na kushinda katika droo inayochezeshwa kila wiki.

Alitoa wito kwa watanzania kujiunga na Y9 microfinance ili kupata huduma za kifedha kwa urahisi pia kujiweka katika nafasi nzuri za ushindi.

Alieleza kuwa sasa tunakwenda ukingoni Kwenye uchezeshaji wa droo hizi tuliahid Kwa watanzania kuwa tutatoa pikipiki 8 na simu 8 hivyo hadii sasa washindi Saba wa pikipiki na wasimu janja wameshapatikana.

Aliongezea kwa kusema "Hadi sasa tumeshatoa zawadi ya pikipiki sita na simu sita na mshindi wa Saba pikipiki na simu wameshapatikana hivyo tumesalia na droo Moja yakutoa zawadi ya pikipiki na simu ili kumamilisha Ile ahadi tuliyotoa".

Mtui amewakumbusha watanzania kuwa "sasa tunakwenda mwisho wakuchezesha droo zetu hivyo niwasihi nduguzangu wakati wako ni sasa tumia App ya Y9 Microfinance ili upate mkopo Kwa njia rahisi pia kujishindia zawadi mbalimbali".

"Baada ya droo yetu ya nane kukamilika tutakwenda kuchezesha droo kubwa ambapo mchindi ataondoka na ndinga mpya kabisa Toyota Ist hii sio ya kukosa endelea kupakuwa app yetu kopa na ushinde".

Alieleza namna ya kushiriki ni rahisi hakikisha umepakua app ya Y9 microfinance kisha kujisajili na kuanza kukopa na moja kwa moja utaingia kwenye droo hii baada ya marejesho.

Kwa upande wake Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi ameeleza "kama bodi ya michezo ya kubahatisha nchini tumeridhishwa na namna ya uchezeshwaji wa droo hii na uhalali katika upatikanaji wa washindi”.

No comments