Breaking News

BARAZA LA FCT LARIDHIA UUNGANISHWAJI WA KAMPUNI YA SARUJI YA TANGA CEMENT NA TWIGA

Mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Tanga cement PLC, Patrick Rutabanzibwa (katikati), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam jana.Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wa pili kulia) na Raymond Mbilinyi, ye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa Tanga Cement pamoja na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement , Quresh Ganijee
Mkurugenzi Mtendaji  wa  Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wapili kushoto), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mwenyekiti wa bodi ya Tanga cement, Patrick Rutabanzibwa, (wa tatu kulia) na Raymond Mbilinyi, ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa Tanga Cement na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement Quresh Ganijee






Baraza la ushindani nchini FCT limeridhia mchakato wa uunganishaji kampunu ya saruji ya tanga na ile ya twiga huku wanahisa wa kampuni ya saruji ya tanga nao wakipitsha maamuzi ya kuruhusu uuzaji hisa asilimia 73 za kampuni hiyo kwenda kwa mwekezaji heidberg ambaye ndiye mmiliki kiwanda cha twiga cement.

Maamuzi hayo yamepitishwa jijini Dare esl saam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa  hisa wa kampuni ya saruji ya tanga Cement ambapo akizungumza Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo patrick rutabanzibwa amesema maamuzi ya wana hisa hao yametokana na hali ngumu inayo ipitia kampuni ya tanga cement ambayo imeshindwa kutoa gawio kutokana na deni ambalo lipo kwenye kampuni hiyo.

Kampuni hiyo pia ilielemewa na gharama kubwa za uzalishaji hivyo kujikuta wakihitaji zaidi uwekezaji kutoka kampuni ya heidelberg inayo miliki kampuni ya scancem ambaye ndie mmiliki wa kiwanda cha twiga cement ili kuingiza nguvu nakuhakikishia wateja kuwa na uhakika wakupata bidhaa hiyo bila kuwa na mashaka.

Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya african mauritus ambaye anamiliki hisa zaidi ya asilimia 73 ya kiwanda cha tanga cement reinhardt swart ambaye ndie mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha tanga cement amesema mchakato wa upatikanaji wa mwekezaji huyo utakamilika haraka iwezekanavyo ili kuongeza nguvu ya uzalishaji wa saruji ambapo pia ameiomba serikali kuimarisha upatikanaji wa nishati kwa uhai wa viwanda nchini

Hata  baadhi ya wana hisa wa kiwanda cha tanga cement ambao wameeleza kusikitishwa na kukosa gawio kwa muda mrefu huku wakibariki kuuzwa kwa hisa hizo na kuunganishwa kwa kiwanda cha tanga cement na twiga cement ili kuwa kiwanda kimoja kitakacho kuwa imara.



WARAKA WA MWEYEKITI

Utangulizi

Wanahisa,

Tuko hapa kuwasilisha taarifa ya biashara iliyokaguliwa ya

Tanga Cement Public Limited Company (“Tanga Cement” au

“Kampuni”) na kampuni zake tanzu (kwa pamoja “Kundi”) kwa

mwaka unaoshia tarehe 31 Disemba 2021.


 Licha ya athari za janga la kimataifa la UVIKO-19, kundi limefanya vizuri kwenye

viashiria vyake muhimu vya utendaji wa kifedha kwa mwaka

ulioishia tarehe 31 Disemba 2021 kama ilivyofafanuliwa

kwenye eneo la mapitio ya Kifedha na Kiutendaji hapo chini.

Tunathibitisha kujitolea kwetu kwa wadau wote kupitia simenti

yetu yenye ubora wa hali ya juu na klinka na pia usambazaji

wetu ambao ni mchango wetu katika ukuaji endelevu na

maendeleo ya Tanzania, kama ilivyo kauli mbiu yetu,


“STRENGTH WITHIN”. Kampuni imeweka viwango vya juu

sana vya afya na usalama katika maeneo yake yote ya utendaji

na inaendelea kutekeleza sera za usalama katika sehemu ya

kazi ili kulinda wafanyakazi wake na wakandarasi.

Mapitio ya Uchumi.


Ukuaji wa kampuni (Kundi) unaendelea kujikita kwenye ukuaji

wa mahitaji ya simenti kwaajili ya soko la ujenzi Tanzania.


Wastani wa kiwango cha mfumuko wa bei kimeongezeka na

kufikia asilima nne nukta mbili (4.2%) mwaka 2021 kutoka

asilimia tatu nukta tatu (3.3%) mwaka 2020. Makadirio ya

ukuaji wa pato ghafi la taifa la asilimia nne nukta tatu (4.3%)

kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia nne nukta nane

(4.8%) iliyorekodiwa mwaka 2020 (kama ilivyochapishwa na

shirika la takwimu la taifa). Japo ongezeko la pato ghafi la taifa

linaridhisha, uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na

uimarishaji wa msingi wa wateja, vinabaki kuwa vichocheo vya

msingi vya ufanisi wa biashara. Mpango wa Serikali wa kati wa

sera za kifedha wenye lengo la asilimia tano (5%) umesaidia

kuongeza uhitaji wa bidhaa zetu. Kampuni (Kundi) inabaki

kuwa na matumaini chanya ya maendeleo chini ya mipango ya

maendeleo ya miundo mbinu iliyopo kwenye dira ya Mpango

wa Maendeleo wa Serikali wa mwaka 2025 na inategemewa

miradi itashika kasi mwaka 2022. Kampuni inaimani na hatua

zilizochukuliwa na Serikali katika kudhibiti maambukizi ya

UVIKO-19 na imedhamiria kufanya kazi pamoja na Serikali

kwenye kukuza uchumi. Kampuni inao uwezo wa kufikia

kiwango maalum cha mahitaji ya simenti nchini na kuendelea

kujizatiti na uzalishai wa bidhaa za simenti zenye ubora wa hali

ya juu. Mapitio ya Fedha na Utendaji Mapato ya kampuni

kutokana na mauzo yaliongezeka kwa kiasi cha asilimia tisa

(9%) na kuwa TZS 231bn kutoka TZS 213bn iliyopatikana


mwaka 2020. Sambamba na ongezeko la mapato, faida ghafi

iliongezeka kwa asilima kumi na nne (14%) na kufikia TZS

61.7bn kutoka TZS 54.2bn iliyopatikana mwaka 2020. Licha ya

miradi mikubwa ya matengenezo ya mitambo yaliyofanyika

mwaka 2021 na kukatika kwa umeme mara kwa mara

kulikopelekea ongezeko la gharama za uzalishaji, pato la jumla

liliongezeka kufikia asilimia ishirini na saba (27%)

ikilinganishwa na asilimia ishirini na tano (25%) ya mwaka

2020.

Kampuni (Kundi) iliingia gharama za mara moja za

marekebisho yaliyosababisha kupungua kwa pato linalotokana

na uendeshaji kwa asilimia kumi na tatu (13%) na kufikia TZS

15bn kwa mwaka 2021 kutoka TZS 17bn kwa mwaka 2020.

Marekebisho hayo ni pamoja na kurekebisha Tanuri (Kiln) na

gharama zilizoambatana na marekebisho hayo ili kurudisha

uzalishaji katika hali ya kawaida. Gharama za kuachana na

operesheni za machimbo/migodi na kuanza kukodi huduma

hizo kutoka kampuni nyingine pia zimechangia kwenye

gharama hizo. Mapato kabla ya Riba, Kodi, Gawio na

Uchakavu (EBITDA) yalipungua kwa asilimia mbili (2%) kufikia

TZS 40.8bn kutoka TZS 41bn iliyopatikana mwaka 2020

iliyosababishwa haswa na gharama za kusitisha mikataba ya

wafanyakazi na gharama za matengenezo ya mitambo.


Kampuni (Kundi) ilirekodi faida kabla ya kodi ya TZS 3.8bn

mwaka 2021 ambayo imeongezeka kutoka hasara iliyopatikana

kabla ya kodi ya TZS 0.63bn iliyopatikana mwaka 2020.

Kuongezeka kwa faida kabla ya kodi ilitokana na kuongezeka

kwa faida ghafi na kupungua kwa hasara zitokanazo na

ubadilishaji wa fedha za kigeni na hasara ya thamani ya fedha

ambazo zinahusiana na deni la mkopo wa ujenzi wa kiln mpya

kuthaminishwa kwa Dola ya Kimarekani (USD) na riba

itokanayo na kukodisha vifaa na mali mbalimbali. Kampuni

iliingia kwenye mkataba mpya uitwao ‘Standstill agreement’

kwenye mkopo wa PIC ambao ulizuia hasara zitokanazo na

ubadilishaji wa fedha za kigeni. Matokeo hayo mazuri

yamechagizwa na kuboreka kwa usimamizi wa hazina, mikakati

ya ununuzi wa fedha za kigeni na viwango vya udhibiti wa mitaji

ya kazi. Kampuni (Kundi) ilipata faida baada ya kodi ya TZS

3.5bn mwaka 2021 ambayo imeboreka kutoka hasara baada

ya kodi ya TZS 2.1bn iliyopatikana mwaka 2020. Fedha taslimu

zilizotokana na shughuli za biashara zilipungua kwa asilimia

hamsini na nane (58%) kutoka TZS 48bn zilizorekodiwa mwaka

2020 na kufikia TZS 20bn mwaka 2021. Mtiririko wa fedha

zilizotokana na shughuli za uendeshaji pia ulipungua kwa

asilimia hamsini na saba (57%) na kufikia TZS 18bn kutoka

TZS 43bn iliyo rekodiwa mwaka uliopita. Mapungufu ya

mtiririko wa fedha yamechangiwa na kushuka kwa faida ya


uendeshaji kwa asilimia kumi na tatu (13%) kutokana na

gharama za mara moja kama zilivyoainishwa hapo juu.

Kuongezeka kwa wadaiwa kwa TZS 5bn, kuongezeka kwa

malighafi kwa TZS 11bn, kupungua kwa madeni ya kibiashara

na madeni ya kimkataba kwa TZS 4bn na TZS 1bn kwa mwaka

2020 na 2021 mtawalia. Kampuni inaendelea kujitoa

kuhakiksha mauzo, ufikishaji bidhaa sokoni na mipango yake

ya kupunguza gharama za uendeshaji vinaendelea kuwa

suluhisho la kuongeza thamani ya wadau wake. Kampuni

inabaki kuwa na matarajio chanya kwa mwaka 2022 licha ya

ushindani mkali na athari za UVIKO-19. Mipango ya Serikali ya

kukuza uchumi kupitia maendeleo ya miundombinu na ukuzaji

wa viwanda vya ndani vinatarajiwa kuchochea uzalishaji wa

ndani wa simenti na matumizi huku ikiendelea kuzuia utitiri wa

uingizaji wa simenti kutoka nje.


Gawio

Kampuni haikutangaza gawio la muda mfupi au la mwisho wa

mwaka kwa wanahisa kwa mwaka 2021 na 2020. Maamuzi

hayo yamefanyika kwa kusudi la kua makini na rasilimali fedha

zilizopo ili kampuni iweze kujikimu na mahitaji mbalimbali katika

kipindi hiki cha kujikwamua kiuchumi kutoka kwenye athari

zilizosababishwa na UVIKO-19. Bodi imeamua kuendelea


kutenga fedha zilizopo kwa ajili ya uendeshaji wa kampuni.

Bodi pia itafanya tathmini ya mwenendo wa kifedha katika

kipindi chote cha mwaka wa fedha wa 2022 kabla ya kufanya

uamuzi wa kutangaza gawio. Pendekezo la kununuliwa kwa

kampuni na Scancem International DA Wanahisa

wanakumbushwa kuhusu tangazo la tarehe 27 Oktoba 2021 la

pendekezo la Scancem International DA kununua asilimia

68.33% ya hisa za Tanga Cement PLC kutoka Afrisam

Mauritius Investment Holdings Limited. Taratibu zote

zinazohusisha mamlaka mbalimbali zimekwisha fanywa. Pande

zote mbili zinasubiri maamuzi ya mamlaka hizo. Wanahisa

wataendelea kupewa taarifa za mchakato huu kadiri muda

unavyoenda.


Hitimisho

Katika kufanyia kazi malengo yake ya muda mfupi na mrefu,

kampuni inaendelea kuwashukuru wafanyakazi wake kwa

mapenzi yao na kujitoa walikokuonesha katika kipindi hiki licha

ya kuwepo kwa changamoto, na pia kwa wateja wake kutokana

na uaminifu wao kwa chapa yetu ya Simba simenti. Pamoja na

Tanzania kubaki kuwa mshirika mkuu katika Jumuia ya Afrika

Mashariki kwenye soko la ujenzi, uzalishaji wa simenti


unategemewa kuongezeka na Kampuni imejiweka tayari

kuchukua fursa hizo za ukuaji wa soko kwenye kanda.

Kwaniaba ya Bodi ya Wakurugenzi

Patrick Rutabanzibwa

No comments