TBS YATOA VYETI NA LESENI ZA UBORA 145 KWA WAJASIRIAMALI NA WAZALISHAJI WA BIDHAA
Na Mwandishi Wetu.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa vyeti na leseni 145 kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023.
Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 17,2023 wakati wa Zoezi hilo lililofanyika katika Ukumbi wa TBS Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga amesema kuwa kati ya vyeti hivyo, vyeti vya ubora wa mifumo (system certification) vilivyotolewa ni sita (6) na Leseni zilizoongezewa bidhaa (Licence extension) ni 13.
Aidha, Bw. Msasalaga amesema kuwa leseni na vyeti 60 ambayo ni sawa na asilimia 43 vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo.“Vyeti na leseni zilizotolewa ni za bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vilainishi, vitakasa mikono, vifaa vya umeme, vifaa vya makenika, vibebeo pamoja na vifungashio”. Amesema
Pamoja na hayo amesema kuwa Jukumu la usajili wa vyakula, vipodozi na majengo limetokana na marekebisho ya sheria ya Viwango yaliyofanywa na sheria ya fedha ya mwaka 2019, na kwa mabadiliko hayo, ‘hakuna bidhaa ya Chakula au vipodozi itakayoruhusiwa katika soko la Tanzania kama haijasajiliwa au kuthibitishwa ubora wake na TBS’ [The Finance Act, section 17 (a) (m)].
“Kwa kipindi cha kuanzia mwezi June mpaka Novemba 2023 tumekwisha sajili majengo -1003- ya biashara na ya kuhifadhia bidhaa za vyakula na vipodozi. Pia kwa kipindi hicho tumeweza kusajili bidhaa 906 za vyakula na vipodozi”. Amesema Bw. Msasalaga
Hata hivyo amewataka wazalishaji wa bidhaa kuzalisha bidhaa zenye Ubora kabla ya kuingiza sokoni ambapo itawasaidia kulinda soko lao kitaifa na kukuza wigo wao wa biashara kutokana na kuwa na alama ya ubora na kulinda afya ya mlaji.
“Unapokua na alama ya ubora ya TBS wateja wetu watapata imani zaidi kwa bidhaa zetu tunazozizalisha na kwa kuwa imani ya walaji inaongezeka utaona zitakubalika sokoni na utapata faida ya Ushindani na utapeleka bidhaa yako yoyote ndani ya Afrika mashariki." Amesema
Kwa upande wake Mjasiriamali wa bidhaa za Choya, Bi.Elizabeth Mtei ameishukuru TBS kwa kuwapatia leseni bure kama wajasiriamali wadogo ambayo imewaongezea wigo wa kuuza bidhaa zao nje ya mipaka ya nchi na amewashauri wajasiriamali wengine kujitokeza TBS kukaguliwa bidhaa zao ili watanue fursa yao kibiashara.
Naye Afisa Masoko wa Kilimanjaro Cable,Bw.David Tarimo amewaasa Watanzania kuamini bidhaa zinazozalishwa katika Viwanda vya ndani kwani TBS na Serikali imewaamini na kuwapatia leseni.
Katika kipindi cha mwaka 2023 TBS ilitwaa tuzo ya Shirika Bora la udhibiti barani Afrika, ambayo imechagizwa na usimamizi mzuri na udhibiti katika kuhakikisha bidhaa ina viwango na ubora unao stahili.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga akikabidhi leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga akikabidhi leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Lazaro Msasalaga akizungumza katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wadau na wazalishaji wa bidhaa nchini wakiwa katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau na wazalishaji wa bidhaa nchini wakiwa katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi June hadi November, 2023. Hafla hiyo imefanyika Novemba 17,2023 katika Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
No comments