OMTO YAPELEKA FURSA YA VICOBA ENDELEVU KWA WATEULE ULONGONI
Mkurugenzi wa Taasisi
ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna
Haule akitoa elimu ya vicoba endelevu kwa wanachama wa Kikundi cha
Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 12
ya kikundi hicho jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi huyo alialikwa kuwa
mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Mwalimu wa Wateule
Vicoba, Glory Munisi akitoa elimu kuhusu elimu ya fedha wakati wa hafla ya
kuadhimisha miaka 12 ya kikundi hicho kilichopo Ulongoni jijini Dar es Salaam
jana. Wateule Vicoba inajumla ya vikundi 7
chini ya ,Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Taasisi
ya Fahari Tuamke Maendeleo, Neema Mchau akizungumza wanachama wa Kikundi cha
Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni kuhusu masuala ya kuthamini familia
pamoja na kuimarisa ndoa wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 12 ya kikundi
hicho jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Wanachama
wa Wateule Vicoba wakisikiliza kwa makini mada zinazotolewa katika maadhimisho
hayo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya
Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna
Haule (katikati), Katibu wa OMTO, Eliwaza Joseph na Mkurugenzi wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo,
Neema Mchau wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza maadhimisho ya
maika 12 ya Kikundi cha Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni jijini Dar es
Salaam jana.
Mkurugenzi wa Taasisi
ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna
Haule ( wa tatu kulia waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
serikali ya mtaa, walimu wa vicoba mbalimbali pamoja na wanachama wa Kikundi
cha Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni baada ya kumaliza hafla ya kuadhimisha
miaka 12 ya kikundi hicho jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi aliahidi
kufanya mipango ya kuvisajili vikundi vyote 7 vilivyopo katika kikba hicho
pamoja na kushirikiano nao ili kupata fursa zilizopo kwenye Vicoba endelevu
kama CRDB Imbeju.
No comments