Breaking News

Tigo Yaja na Chapa Mpya


 

Honora Tanzania Public Limited (“Tigo”) na Honora

Tanzania Mobile Solutions Limited (“Tigo Pesa”), ambazo ni sehemu ya kampuni ya AXIAN Telecom

Group zinatangaza mabadiliko makubwa ya chapa ambapo Tigo itajulikana rasmi kama Yas, huku

huduma zake za kifedha, Tigo Pesa, zikibadilishwa kuwa Mixx by Yas. Hatua hii muhimu katika historia

ya kampuni, na inaakisi azma yake ya kuendeleza ubunifu wa kidijitali na ujumuishaji wa Watanzania

kwenye huduma za kifedha.

Mabadiliko haya ya chapa ni sehemu ya mpango mkakati wa AXIAN Telecom wa kuunganisha


makampuni yake yote ya mawasiliano barani Afrika kuwa chini ya chapa moja, Yas na Mixx by Yas kama

alama ya nguvu ya Pamoja na mafanikio.

Yas na Mixx by Yas, zinalenga kuakisi maono ya kampuni ya kuwa kiini cha mapinduzi ya kidijitali barani

Afrika. Kupitia suluhisho za kisasa za kidijitali na kifedha, chapa hizi mpya zinalenga kuboresha maisha ya

mamilioni ya Watanzania na kutoa fursa mpya zisizo na kikomo.

Rostam Azizi, Mwenyekiti wa Bodi ya Yas Tanzania, alisema;

“Yas ni ishara ya nguvu tuliyonayo Afrika. Mabadiliko haya yanaonesha dhamira yetu ya kuendelea

kuwekeza na kuleta mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania, bara na Visiwani. Tukishirikiana na Axian

Telecom Group, tumejipanga kutengeneza fursa mpya, kuhamasisha ubunifu, na kujenga mustakabali

bora ulio na lengo la kuimarisha sekta ya mawasiliano.”

Hassanein Hiridjee, Mwenyekiti wa Bodi ya Axian Telecom Group, alisema:

“Axian Telecom imekuwa katika safari ya kipekee ya kuunganisha watu barani Afrika kupitia chapa zetu.

Kadri tunavyopanua wigo wa humuma zetu, tunaendelea kuyafikia maono yetu ya kuwa kampuni ya

mawasiliano inayotoa hukduma kwenye nchi nyingi zaidi barani Afrika. Tunapozindua chapa mpya ya

Yas, tunalenga kuunganisha bara hili kwenye fursa mbalimbali. Tunaamini Yas itaendeleza mafanikio na

utamaduni wetu huku ikitoa suluhisho jumuishi na endelevu za kiteknolojia.”

Jerome Albou, Kaimu Afisa Mkuu wa Yas Tanzania, aliongeza:

“Leo ni siku ya kihistoria kwa kampuni yetu. Kama Yas, tumejipanga kuwa mshirika wa maendeleo,

tukiwapa nguvu wateja wetu na kuwahakikishia kuwa biashara zitastawi katika mazingira yenye

ushindani mkubwa. Hivyo basi tutaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa, huduma bora kwa

wateja huku tukiendelea kuwekeza kwa vijana ambao ni msingi wa maendeleo ya baadaye ya Tanzania.”

Mbali na kuunganisha chapa zake za makampuni ya mawasiliano , Axian Telecom pia inaunganisha

huduma zake za kifedha nchini Togo, Senegal, na Tanzania chini ya chapa ya Mixx by Yas . Lengo ni

kuboresha uzoefu wa wateja kwa kushirikiana zaidi kati ya nchi hizi. Huduma za kifedha kwa njia ya simu

za mkononi ni eneo muhimu la ukuaji kwa kampuni barani Afrika, ikibaki mstari wa mbele katika

ujumuishaji wa kifedha.

Mabadiliko haya yanaonesha azma ya Axian Telecom Group ya kuendelea kuboresha huduma zake kwa

kutumia teknolojia, ili kuwahudumia wateja wake vyema zaidi na kufanikisha maendeleo endelevu

barani Afrika.

 

Yas Tanzania (zamani Tigo Tanzania) ni kampuni ya mawasiliano na teknolojia ya kidijitali anayeongoza

nchini Tanzania. Kwa zaidi ya miongo mitatu, Yas imekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma za

kifedha kupitia simu za mkononi, ikihudumia wateja zaidi ya milioni 23 kote nchini. Ikiwa sehemu ya

Axian Group—kinara wa huduma za mawasiliano barani Afrika—Yas inaongoza kuwa na mtandao mpana

wa 4G unaounganisha Watanzania kila kona ya nchi Pamoja na 5G yenye kasi zaidi. Huduma za kifedha

kupitia simu za mkononi za Mixx by Yas zinaendelea kuwezesha ndoto za watanzania kwa kuwa ni

salama, na zinazopatikana kwa urahisi kila kona ya nchi.













 

No comments